Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Spika wa Bunge, Job Ndugai (Mb) amemuapisha Mbunge wa kuteuliwa Mchungaji Getrude Rwakatare leo Bungeni Mjini Dodoma.
Mama Rwakatare amepata nafasi ya uteuzi huo baada ya Chama Cha Mapinduzi CCM kumfuta uanachama aliyekuwa Kiongozi wa UWT, Bi. Sophia Simba hivyo kwa mujibu wa sheria za uchaguzi Sophia Simba akapoteza sifa ya kuwa Mbunge kwakuwa si Mwanachama wa chama chochote. Hivyo Tume ya Taifa ya Uchaguzi ikamteuwa Mchungaji Rwakatare kuchukua nafasi hiyo.