Mchungaji Peter Msigwa wa CHADEMA akamatwa na Jeshi la Polisi.

kuna kipindi hekima,busara na maarifa hazinabudi kutumika,kuna vitu watu wanaweza kukaa chini na kuelewana
pasipo kutumia nguvu!
 
kimsingi nadhani imefika wakati ambapo watu husani viongozi wanatakiwa kutatua matatizo ya watu kwa maono ya mbali. nadhani ni pande zote zina wajibu wa kukaa na kuangalia ni vipi suala hili la wamachinga linatatuliwa kwa manufaa ya wamachinga wenyewe,halmashauri na taifa kwa ujumla. wamachinga wapo si iringa pekee ni ulimwengu mzima suala serikali kuweka mazingira stahiki na bora kwa kazi zao.serikali inaileza changamoto ya ajira kila kukicha lakini kwa nchi zinazoendelea wafanyabiashara wadogo na biashara ndogondogo ndiyo fursa ya awali ya utatuzi wa tatizo la ajira. kuwafukuza au kuwahamisha wamachinga kwa kigezo cha kusafisha mji c hoja yenye uzito kulinganisha na utafutaji ridhiki na hali ya uchumi wa mtanzania wa kawaida. tunasafisha miji kwaajili ya nani? mji uwe safi huku wananchi wana njaa? au niamini ni tabaka fulani la watu ambao kutafuta ridiki kwa umachinga ni uchafu na uhalifu? HII IMEPELEKEA HATA WALE WANOONA FURSA YA KUJIONGEZEA FURSA KATIKA SHUGHULI ZAO KUJIPENYEZA KIRAHISI. SISEMI NI HALALI KUTAFUTA RIDHIKI BILA KUFUATA UTARATIBU, ILA TARATIBU ZINAZOWANYIMA WATU KUTAFUTA RIDHIKI NI KWAAJILI YA NANI? ILHALI TUNASEMA TUPO KWAAJILI YA USTAWI WA WATU WETU NA WAMACHINGA WAKIWEMO. HALMASHAURI YA MANISPAA IMESHINDWA KUZIONA FURSA AMBAZO ORDINARY CIVILIANS(WAMACHINGA WAMEZIONA) KWA KUSHINDWA KUANDAA MAZINGIRA BORA ILI NAYO IPATE CHANZO CHA MAPATO KWA SHUGHULI NDOGO KAAMA ZA USAFI NA NYINGINEZO. TAIFA HALIWEZI PIGA HATUA KAMA HATUTAPATA VIONGOZI WENYE AKILI NA MITAZAMO YA MBALI. BAADALA YAKE KILA MTU ATAJISHUGHULISHA YE NI MWAMBA KIASI GANI. TUNASHINDWA KUPAMBANA NA CHANGAMOTO ZA KITAIFA VIPI KUHUSU ZA KIMATAIFA

mkuu Kelvin KIHWELU ni vile natumia tu simu ila bandiko lako linahitaji like yangu,ila pokea like yangu juu kwaju mkuu
 
Last edited by a moderator:
Kwanini mtaji wa
popularitization kwa cdm ni vurugu? Watanzania shitukeni hiki sio chama
cha maendeleo ila kurudisha nyuma taifa.

Hv Iringa ndo police wanahistoria ya kuuwa mwandishi sio? mmh kumbe huyu Gamba najua hatanielewa,magamba ni wagumu hawa kuelewa.Siasa zao n bora ufe kwani unawakera.
 
Yeeees that is a wise decision, bora kumkamata msababishaji wa vurugu kuliko kupambana na wafanya vurugu.

Kama kasababisha vurugu subiri ashtakiwe na siyo hii ya kuwakamata kila kukicha then inashia hewani wakidhani wanawamaliza kisiasa kumbe ndo kwanza wanapaisha
 
Siko humu JF kukufurahisha wewe au mtu mwingine yoyote.
Niko humu JF kutumia akili na uhuru wangu katika kuwasilisha mawazo yangu ambayo yana-reflect mawazo ya watanzania wengi wenye Hekima.
Nahisi unanichukia kwa sababu mimi sio mwanaCCM au mwanamtandao wa CCM Lumumba wanaolipwa 7000 kwa siku kuja kupost mashudu humu JF.
Kama post zangu zinakuumiza sana, ninakushauri uache tu kuzisoma.

*Turudi kwenye mada:
1/Maandamano ni tukio la Haki na Amani popote pale duniani. Inakuwaje mtu adai Kufanya maandamano ni kuvunja sheria au kuleta vurugu?

2/Kwa sheria za Tanzania, hauhitaji kibali ili uandamane na wala huhitaji ruhusa kutoka jeshi la polisi ili uindamane. Maandamano ni haki ya msingi ya mtanzania yoyote inayotajwa kikatiba.
Jeshi la polisi linahitaji kutaarifiwa tu ili lije kulinda maandamano yako. Na usipolitaarifu jeshi la polisi, maana yake maandamano yako yanaweza kukosa Ulinzi wa Polisi tu. Ni makosa makubwa kwa jeshi la polisi Tanzania kuzuia maandamano yoyote mahali popote.

JF imeingiliwa na watu wenye IQ ndogo sana kwa kweli!

Mijadala ya humu ilikuwa genuine, tunatoa hoja na kujibu kwa hoja, now days tunaona mipasho tu.

Sidhani kama unajua dhana nzima ya kuomba kibali, katiba ya nchi imehalalisha maandamano, ni sawa, lakini kuna taratibu zimewekwa ili uhalali huo wa katiba ukamilike.

Na utaratibu wa kibali vilevile unaambata na ulinzi kama ulivyo sema, sasa kwanini hawa wamachinga wamekiuka kupewa ulinzi wa polisi?

Mambo mengine huna haja ya kuyawekea ubishi mkuu, ni kukubali kuwa Msigwa amekosea kutoa baraka zake kwa namna ya kuhamasisha hayo maandamano yasiyo na kibali.
 
kwa ccm ukitetea wanyonge au rasilimali za nchi unaonekana unafanya vurugu na kuvunja amani ,ccm ni watetezi wa uhalifu duniani kwa mfano,bus moja la buffalo lilikamatwa masasi tangu mwaka juzi kwa kosa la kukutwa meno ya tembo vipande ndani yake hadi leo lipo polisi masasi je? mmiliki anakosa? kwanini asipewe bus lake kama akina kinana walivyoachiwa meli yao? bus lake kazi yake kusafirisha abiria kwanini limezuililwa? majibu yanahitajika kwenu policcm!!
 
viongozi kama msigwa kunahaja gani ya kuwa nao inakuwaje mtu analazimisha wafanye biashara hadi barabarani halafu achwe tu hii siyo sawa tena polisi walipaswa kumpiga hata risasi kwa kweli hana maana na hafai.
 
Mtumwa ni wewe ambaye muda wote unatetea kila kitu CDM wanachokifanya hata kama ni cha kipuuzi. Inabidi mkuu ubadilike, jifunze kuwa na mawazo huru. Kwa stahili hii CDM hawajengi bali wanazidi kubomoa na kujichimbia kaburi lao wenyewe!
Kuliko Hilo ccm ambalo wameshajichimbia?
 
kwa ccm ukitetea wanyonge au rasilimali za nchi unaonekana unafanya vurugu na kuvunja amani ,ccm ni watetezi wa uhalifu duniani kwa mfano,bus moja la buffalo lilikamatwa masasi tangu mwaka juzi kwa kosa la kukutwa meno ya tembo vipande ndani yake hadi leo lipo polisi masasi je? mmiliki anakosa? kwanini asipewe bus lake kama akina kinana walivyoachiwa meli yao? bus lake kazi yake kusafirisha abiria kwanini limezuililwa? majibu yanahitajika kwenu policcm!!

umefuatilia polisi masasi ukajua maelezo ya hiyo kesi yapoje au unaongea tu kwa sababu umepata mda wa kuongea.
 
Mkuu mimi binafsi huyu Msigwa nashindwa kumuelewa
Anafanya vurugu kwa makusudi ili na yeye aandikwe kama yule kubwa jinga wa Arusha.
Anyway, mwisho wake ni 2015 kwani nitahakikisha anarudi kuuza kisosk pale kihesa
Acha kuandika ujinga humu JF.
Kama una ujasiri njoo hapa Arusha mjini au nenda pale Iringa mjini halafu useme hayo maneno yako.

Wewe ni mtu mzima na uko huko UK lakini akili yako bado ni ndogo kuliko hata bata anayefugwa kule Mahenge.

Mtu mzima hovyooo!!!
 
pole sana mtetez wa wanyonge, msema kweli sikuzote hubezwa maana kufanyia biashar kwa siku moja kunaathir nn na uzingatia mashine 3road not buss road like main roads. Hawatendi haki kwa machinga na wa2 wengine.
 
mambo mengine ya ni ya kikoloni sasa.miji yote wamachinga hufanya biashara minjini kwani ndio eneo lenye watu.wamachinga hutegemea watu ili wafanye biashara.ni vyema wakasikilizwa pia.mfano manispaa ya moshi kuna kipindi walifunga baadhi ya njia za magari na kuwaweka hao wamachinga wafanye biashara.

mkuu umesema ukweli na ndilo jambo la busara ambapo kwa serikali yeyote sikivu na yenyekupenda maendeleo ya raia wake ingepaswa kufanya ila kwavile serikali yetu inaangalia lile jimbo nila nani then ndo wanafanya uamuzi basi tutegemee haya kuendelea kutokea mara kwa mara
 
Nilikuwa nategemea akae na hao machinga awaelimishe namna ya kuheshimu mamlaka, kama anawafundisha namna ya kupingana na mamlaka anakosea sana. Dini kazi yake ni kuleta amani na siyo machafuko

Dhulma ya watawala ni chukizo mbele za mungu,

Waamini wasimamie haki zao bila kujali hiyana na mumiani bali angalizo la Mungu tu!
 
Back
Top Bottom