Mchungaji Msigwa: Waziri Mkuu Majaliwa ni kiongozi shupavu anayestahili kupigiwa mfano

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,975
Mbunge wa Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa amemmwagia sifa lukuki waziri mkuu mh Majaliwa aliyeko ziarani mkoani Iringa.

Mbunge Msigwa amesema waziri mkuu mh Majaliwa ni kiongozi msikivu anayefundisha, anayekemea palipoharibika na kupongeza pale panapostahili pongezi hivyo Chadema mkoa inamuunga mkono.

Msigwa ameyasema hayo katika mkutano wa waziri mkuu na viongozi wa kisiasa na watendaji wa serikali mkoani Iringa.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Hongera sana Mchungaji Msigwa kwa ujasiri huo wa ‘kuchezea gego la simba’ maana huko ulipo kusifia Serikal ni zaid ya uhaini
 
Mbowe atampigia simu sasa hv, atamwambia, wee Mchungaji umejisahau au una malengo gani? Si tulikubaliana tuipinge serikali ya CCM kwa kila kitu?
 
Mbowe atampigia simu sasa hv, atamwambia, wee Mchungaji umejisahau au una malengo gani? Si tulikubaliana tuipinge serikali ya CCM kwa kila kitu?
Nimekumbuka wale wabunge wengine Wa ccm naunga mkono 100% kwa 100% wamezoea vivo.
 
Mbowe atampigia simu sasa hv, atamwambia, wee Mchungaji umejisahau au una malengo gani? Si tulikubaliana tuipinge serikali ya CCM kwa kila kitu?
Hayo ni mawazo yako ya kijinga tuu. Kama unamsikiliza Majaliwa huwa hana ulimbukeni walio nao bosi wake na baadhi ya watendaji wa hovyo wengine.
Msigwa alichofanya ni Kum pre empty Magu na wengine aina ya RC Happi na wenye akili wameelewa hivyo. Wewe na wenzako sijui tuwasaidieje kama hamuwezi kuelewa!
 
Back
Top Bottom