Mchungaji Msigwa kizimbani, asomewa mashtaka

Mchungaji Msigwa kizimbani, asomewa mashtaka

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
26,692
Reaction score
59,194
msigwa.jpg


Mgombea ubunge katika Jimbo la Iringa Mjini kwa tiketi Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mchungaji Peter Msigwa na watu wengine watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Iringa leo na kusomewa mashtaka manne, ikiwemo la uvunjivu wa amani.


Hata hivyo, wengine sita hawakuweza kufika mahakamani hapo leo lakini mahakama hiyo imeelezwa kuwa washitakiwa hao wataunganishwa katika kesi hiyo.

Mbali na uvunjifu wa amani, mwanasiasa huyo machachari na wenzake wanakabiliwa na makosa mengine yakiwemo kuharibu mali na kujeruhi polisi.

Hata hivyo, Msigwa na wenzake wameyakana mashtaka yote waliyosomewa leo na kuachiwa baada ya kukidhi vigezo vyote vya kupewa dhamana. Kesi yao itatajwa tena Novemba 2, mwaka huu.

Mwishoni mwa mwezi uliopita, Mchungaji Msigwa alikuwa ni miongoni mwa wafuasi 64 wa Chadema walitiwa mbaroni na kulala rumande usiku mmoja.

Chanzo: Mwananchi
 
Bado hakuna unafuu kwa ccm iringa mjini
 
Ndio maana nasema huyu Mchungaji fake kabisa Kwakuwa anakiuka kanuni na sheria za wachungaji....
 
Lakini twende mbele na kurudi nyuma ili kuweka kumbukumbu sawa. Iringa ni kati ya sehemu chache duniani iliyoingia kwenye rekodi ya mapambano ya kidemokrasia kwa ushahi wa kuuawa mwandishi wa habari akihoji juu ya haki na usawa kwa viongozi wa dola.

Hili la Msigwa ni kutaka kutumia kodi zetu vibaya kwani hakuna kosa alilotenda moja kwa moja na hata ushahidi ni dhaifu. Ni kwanini wanasheria wakubali kupoteza nguvu na muda kwenye mashauri yasiyokuwa na maslahi kwa umma?

Hebu busara ya kawaida tu itumike kuona jinsi ya vyombo vya dola kutumika pasipo mashinikizo ya kina Lukuvi, Nape na Mwigulu ili wasiivuruge amani na waache tamaa ya madaraka kwani si lazima kuongoza watu wasiohitaji uongozi wako.

Na vyombo vya dola viwe vinabalance siasa ili kuleta fairness badala ya kutumika kwa chama fulani..
 
Wanamabadiliko mliko Iringa mpeni kura za kutosha Msigwa ashinde tena haijalishi kama ataapishwa akiwa Magereza. Waadabisheni ccm mjini hapo tuone kama hawajaikimbia hiyo kesi ya kimagumashi.
 
Insanity is keeping doing the same thing the same way and expecting different result.... mwqka 2010 mwakalebela alifunguliwa kesi msigwa akashinda leo msigwa kafunguliwa kesi makalebela atadindaa??
 
Hizo ni kesi za kisiasa na huisha juujuu tu. Lengo ni kupotezeana muda na kuacha kujadili mambo ya msingi.
 
Hawa watu bwana hawataki Kabisa kuelewa kuwa sasa imefika mwisho tunasema CCM no
 
Back
Top Bottom