Mchungaji Msigwa afikishwa mahakamani, apatiwa dhamana

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
WhatsApp Image 2018-01-24 at 4.06.16 PM.jpeg

CHINI YA ULINZI: Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa (CHADEMA) na wenzake 12 wamefikishwa ktk Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa kwa tuhuma za kuchoma nyumba ya Katibu wa UVCCM mkoani humo na kubomoa nyumba ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwangata aliyehamia CCM, Angelus Lijuja.

Polisi walijaribu kama kawaida yao kuzuia dhamana zao kwa kiapo cha RCO lakini Mahakama imetupilia mbali kiapo hicho na imewapatia dhamana .

Wameshitakiwa kwa makosa yanayoitwa eti kula njama za kuharibu mali na kuvunja na kuchoma nyumba ya kada wa UVCCM Moto , Haya yana mwisho.

=====

Mh Peter Msigwa na Viongozi 12 Wa Chadema Wapata DHAMANA Mahakamani*

Waliofikishwa Mahakamani ni:-

1. Peter Msigwa
2. Leonce Marto
3. Samwel Nyanda
4. Adrey George Mkemwa
5. Rehema Mbetwa
6. Maneno Rashid Mbuma
7. Rody Jumanne Makimwa
8. Deogratius Faustine Kisumi
9. Patrick Madat
10 Luioniso Kadaga.
11. Gama Msigwa

Walifikishwa Mahakamani kwa
*Makosa*
1. Kula njama kutenda kosa la kuleta madhara kwenye mali.

2. Uharibifu wa mali. Kati ya tarehe 15/1/2018 waliharibu nyumba ya Anjelus Lijuja yenye thamani ya million saba.

*KIAPO CHA MPELELEZI WA MKOA*

Mwendesha mashtaka ameleta ombi kwamba washtakiwa wasipewe dhamana kwa kulinda usalama wao. Wabakie ndani hadi hapo upelelezi utakapokua umekamilika. (sect. 48 mwenendo wa dhamana)

Wakili: hatujapokea hicho kiapo na hatujui kilichopo ndani. Ifahamike suala la dhamana ni haki ya mtuhumiwa na siyo priviledge. Its a right. Madhumuni yake yako wazi kutokana na kanuni ya presumption of innocent. Watuhumiwa bado hawajahukumiwa kutenda kosa. (Reference of other reported cases to support the defence)

Mahakama imetupilia Mbali Kiapo hicho na kutoa dhamana kwa watuhumiwa

Hata Jeshi La Polisi Mkoa Iringa Bado linamshikilia Mwenyekiti wa Bavicha wilaya kilolo Mwalimu Kuzen Msungu na Limeshindwa kumfikisha mahakamani pamoja na watuhumiwa Wezake,

Tunatoa wito kwa jeshi la Polisi Kama linaona hakuna sababu ya kupeleka mahakamani Kamanda Msungu Limwachie

Tunatoa Pongezi kwa Viongozi,wanachama ,na wafuasi wa chadema kwa kuonesha ushirikiano,Umoja na Mshikamano

_imetolewa na_

*JACKSON MNYAWAMI*
*KATIBU WA BAVICHA*
*MKOA WA IRINGA.*

Habari zaidi soma=>Mbunge wa Iringa mjini, Mchungaji Msigwa akamatwa na Jeshi la Polisi na kupelekwa mahabusu
 
Jaji mkuu siamesema mahakama isiingiliwe?sijui ndio maana wamapata ahueni hapo,au hakimu kaamuatu
 
Tokea mfumo wa vyama vingi uingie utawala huu wa awamu ya tano umewafikisha mahakamani viongozi wa upinzani wengi sana kwa kipindi cha miaka miwili kuliko waliofikishwa kipindi cha miaka ya Mwinyi, Mkapa na JK.
Wenye akili walipaswa kujiuliza kulikoni huyu jamaa?
Pengine ni ule ushamba na ulimbukeni aliosema Zitto, au woga kwa kushindwa kuongoza na pengine basi yaweza kuwa ana kitu anaficha na anatumia nguvu nyingi kisifahamike
 
CHINI YA ULINZI: Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa (CHADEMA) na wenzake 12 wamefikishwa ktk Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa kwa tuhuma za kuchoma nyumba ya Katibu wa UVCCM mkoani humo na kubomoa nyumba ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwangata aliyehamia CCM, Angelus Lijuja.
======================================================

Hatimaye Rev.Msigwa na viongozi wengine 13 wamepandishwa kizimbani leo katika Mahakama ya Iringa , polisi walijaribu kama kawaida yao kuzuia dhamana zao kwa kiapo cha RCO lakini Mahakama imetupilia mbali kiapo hicho na imewapatia dhamana .

Wameshitakiwa kwa makosa yanayoitwa eti kula njama za kuharibu mali na kuvunja na kuchoma nyumba ya kada wa UVCCM Moto , Haya yana mwisho
Umenikumbusha Zombe na wafanyabiashara ya madini kule mabwep.....!!
 
Ukiona hivyo demokrasia nchini inapata mizizi yake. Siasa si kwa watu wanaojaribu ni kwa watu waliodhamiria kama akina Nyerere, Babu, Mandela, Nkrumah, Lumumba, Kenyata, Lissu, etc.
 
Msihuzunike wala kubabaika kuwa mtesema nini dhidi ya watesi wenu, 'tazama baba yenu wa mbinguni atawapa Roho Mtakatifu na atanena kwa niaba yenu'. Basi mtumainieni yeye kwani yote yatapita kwa jina lake na haki itatamalaki.
 
Amen
 
Tokea mfumo wa vyama vingi uingie utawala huu wa awamu ya tano umewafikisha mahakamani viongozi wa upinzani wengi sana kwa kipindi cha miaka miwili kuliko waliofikishwa kipindi cha miaka ya Mwinyi, Mkapa na JK.
Wenye akili walipaswa kujiuliza kulikoni huyu jamaa?
Pengine ni ule ushamba na ulimbukeni aliosema Zitto, au woga kwa kushindwa kuongoza na pengine basi yaweza kuwa ana kitu anaficha na anatumia nguvu nyingi kisifahamike
Hata ningekuwa mimi , kupata kura mil 3.5 dhidi ya kura mil 10 ilikuwa aibu sana !
 
Lockup za iringa funga Msigwa nywele Kama kichaa katoka kichakani kawa mweusi kuliko RAIA wa Sudan kusini.
 
Lile onyo la Jaji Mkuu mahakimu wenye weledi na kazi yao wanalifanyia kazi kwa weledi.
Hakimu hajafanya kwa weledi hao waliochomewa nyumba Polisi wameona wanaweza mfanyia kitu mbaya Msigwa. Hakimu alitakiwa alizingatie hilo
 
Hicho kiapo ambacho wakili wa Msigwa alisema hatujakiona hakimu alitakiwa amwambie mwendesha mashtaka wahi mwonyeshe chap chap sasa hivi au angesema hii kesi naiahirisha hadi mwendesha mashtaka atakapompelekea kiapo wakili wa utetezi akisome akielewe kwa Leo naamuru Msigwa na kundi lako mrudi rumande hadi siku ingine Simple.Sikubaliani na hakimu alichoamua
 
Bado hakimu mkazi wa mbeya, mtaita siku zake zinahesabika nakuambia.
 
Hicho kiapo ambacho wakili wa Msigwa alisema hatujakiona hakimu alitakiwa amwambie mwendesha mashtaka wahi mwonyeshe chap chap sasa hivi au angesema hii kesi naiahirisha hadi mwendesha mashtaka atakapompelekea kiapo wakili wa utetezi akisome akielewe kwa Leo naamuru Msigwa na kundi lako mrudi rumande hadi siku ingine Simple.Sikubaliani na hakimu alichoamua
Una maanisha ulichoandika au unatania?
 
Una maanisha ulichoandika au unatania?
Hajampa muda wakili wa Serikali kuwakilisha hicho kiapo au hata angeuliza unasema hujampa ni kweli na kama hujampa kwa nini?Hukumu imeegemea upande wa wakili wa utetezi tu sioni hakimu akiuliza hayo maswali
 
Lockup za iringa funga Msigwa nywele Kama kichaa katoka kichakani kawa mweusi kuliko RAIA wa Sudan kusini.
Kauli chafu kama hizo alikuwa nazo Zombe lakini mpaka muda huu anapigania roho yake .
 
Hicho kiapo ambacho wakili wa Msigwa alisema hatujakiona hakimu alitakiwa amwambie mwendesha mashtaka wahi mwonyeshe chap chap sasa hivi au angesema hii kesi naiahirisha hadi mwendesha mashtaka atakapompelekea kiapo wakili wa utetezi akisome akielewe kwa Leo naamuru Msigwa na kundi lako mrudi rumande hadi siku ingine Simple.Sikubaliani na hakimu alichoamua
Hakimu Uchwara wewe.!
 
Back
Top Bottom