Mchungaji Matsahi amtaka Spika Tulia kukaa karibu zaidi na Mungu wakati huu na asiruhusu marafiki wasioeleweka kumkaribia!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,149
Ni ibadani KKKT Kimara ambapo Spika wa Bunge la JMT mh Dr Tulia PhD amejumuika na Wakristo wenzake Jumapili Hii ya Kwanza ya Majilio

Mchungaji Matsahi amemtaka Dr Tulia PhD kuwa karibu zaidi na Mungu wa Mbinguni wakati huu

Aidha amemtaka awe mwangalifu na Marafiki na Watu wanaomsogeleasogelea na iliwezekana awaepuke kabisa

Nawatakia Majilio Yenye Baraka 😀
 
tunapaswa kuwa karibu na Mungu wakati wote.

Amwambie pia, Watanzania wengi ni masikini na chanzo chake ni CCM na watu wake.

Amwambie pia, wakati yeye anatembelea gari la kifahari kwa kodi za wananchi, kuna shule watoto wanakaa chini, kuna hospitali hazina dawa, kuna kaya hazina chakula, Hapo hapo kimara kanisani mita chache watu wanakaa kwenye slum (tumeshindwa kupanga miji), hapo hapo kimara kanisani akitoka muonyeshe hiyo barabara haina taa na kila kitu kiko hovyohovyo...

Kifupi tuwaambie ukweli hawa viongozi wanapokuja kwenye nyumba za ibada, labda wanaweza kukumbuka kuwa wapo kwaajili ya kutumikia wananchi na sio favor wao kututumikia sisi.
 
Ni ibadani KKKT Kimara ambapo Spika wa Bunge la JMT mh Dr Tulia PhD amejumuika na Wakristo wenzake Jumapili Hii ya Kwanza ya Majilio

Mchungaji Matsahi amemtaka Dr Tulia PhD kuwa karibu zaidi na Mungu wa Mbinguni wakati huu

Aidha amemtaka awe mwangalifu na Marafiki na Watu wanaomsogeleasogelea na iliwezekana awaepuke kabisa

Nawatakia Majilio Yenye Baraka 😀
Habari mbaya sana kwa Lucas Mwasambwanda...kila sikuTulia ..Tulia..Tulia....
 
Hizi Dini hizi...., Yaani kabisa mtu wa upendo unashauri watu kukaa mbali / kuepuka wengine ?; Kama huku ndio kuokoka / uokovu bora nipotee tu....

watu tunajitahidi kujenga maradaja wao wanataka tujenge kuta.... (kujitenga)
 
Naheshimu sana viongozi wa dini ila kuna wakati kweli siasa na wanasiasa wawaache tu. Kiongozi aliyewekwa na watu anakaaje mbali na watu? Yaani wajinga na werevu wote ni wake,alichopaswa kumfundisha labda ni hekima ya kimungu ya kuishi maisha yake kama kiongozi ila si kumfundisha ubaguzi. Tulia ukimuondoa Uspika na ubunge ni muumini kama waumini wengine na pengine ibada ilipaswa isisitize hilo kuwa mbele ya madhabahu wote wenye vyeo na wasiokuwa navyo ni sawa mbele za Mungu. Kazi sana,ubinadamu huu kazi sana.
 
Ni ibadani KKKT Kimara ambapo Spika wa Bunge la JMT mh Dr Tulia PhD amejumuika na Wakristo wenzake Jumapili Hii ya Kwanza ya Majilio

Mchungaji Matsahi amemtaka Dr Tulia PhD kuwa karibu zaidi na Mungu wa Mbinguni wakati huu

Aidha amemtaka awe mwangalifu na Marafiki na Watu wanaomsogeleasogelea na iliwezekana awaepuke kabisa

Nawatakia Majilio Yenye Baraka 😀
sawa
 
Back
Top Bottom