Mchungaji wa kanisa la Evangelical Asemblies of God katika kijiji cha Ntuchi Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa, Evans Kankoma (41) anatuhumiwa kumbaka mtoto wa miaka mitano mwanafunzi wa darasa la kwanza.
Kwa muijibu wa taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na ofisa mtendaji wa kijiji hicho, Robert Lunyelele, kiongozi huyo wa kiroho anadaiwa kumfanyia unyama huo mtoto huyo saa 7 mchana kwenye bustani ya miti na matunda.
Inadaiwa mtoto huyo na wenzie walikuwa wakitoka shule na walipitia kwenye bustani hiyo kuchuma mapera, Lunyelele alidai kuwa mchungaji huyo alimwita mtoto huyo huku akimlazimisha na kumwamuru mwanafunzi aliyekuwa nae kwenda nyumbani na ndipo alipoanza kumbaka mtoto huyo na kumsababishia maumivu makali.
Alidai mwanafunzi mwenzie aliyeamriwa na mchungaji huyo kwenda nyumbani ndiye aliyetoa taarifa hizo ndipo wazazi wa mtoto huyo anayedaiwa kubakwa walipofatilia kwenye bustani hiyo na kumkuta mchungaji eneo la tukio huku mtoto huyo akilalamika kupata maumivu makali.
Wazazi hao walipiga kelele zilizosababisha watu kufurika eneo hilo.
Baada ya polisi kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa.
Source: Habari Leo tar 04/06/2015