Mchungaji wa Kanisa la Tanga Pentecostal Asemblies of God (TPAG) la jijini Tanga, Jeremiah Kihali, ametia neno kuhusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2025.
Akiongea baada ya ibada ya Jumapili iliyopita, Mikanjuni jijini hapa, Kihali alisema anatoa wito kwa wadau wa amani na serikali kwa ujumla wake kuunga mkono Tamasha la Kuombea Uchaguzi Mkuu 2025 linaloandaliwa na Alex Msama.
Soma, Pia: Alex Msama atangaza Tamasha la kuombea Uchaguzi Mkuu, litafanyika Aprili 20, 2025
Alisema ipo mifano mingi duniani kwamba baada ya chaguzi, nchi zilibaki na majeraha yaliyotokana na mitafaruku mbalimbali.
Kwa hiyo, kwa Tanzania ili kupita salama katika kipindi hicho, ni muhimu kwa waumini na viongozi wa dini zote kumlilia Mungu kwa bidii ili roho ya machafuko isitawale kwenye uchaguzi wa mwaka huu.
"Alex Msama amepata maono mazuri na makubwa kuhusu uchaguzi wa mwaka huu. Hata mimi niliwaza tangu mwaka jana kumbe kuna mwingine aliwaza kama mimi na kufanyia kazi," alisema mchungaji huyo.
Aliongeza kusema kuwa, aliwahi kumsikia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, katika moja ya hotuba zake akisema mwaka huu ni wa uchaguzi, kwa hiyo kuna mambo mengi hutokea.
"Rais Samia katika kauli yake alitumia uzoefu wake. Hata mimi najua. Watanzania wote wanajua, chaguzi nyingi za nyuma hutokea matukio ya kila namna ambayo siyo mazuri.
"Kwa hiyo, kuombea Uchaguzi Mkuu ni maono mazuri sana kwa nchi yetu ambayo amani ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Uchaguzi uje, upite na kutuacha tukiwa bado tumeshikamana," alisema mchungaji Kihali.
Akatoa wito: "Nawaomba wadau mbalimbali, hasa wafanyabiashara, wamdhamini Msama. Amani ya nchi yetu hata wao inawahusu kwa sehemu kubwa kuwasaidia kufanya biashara zao katika mazingira ya amani na utulivu uchaguzi ukiwa umeshapita salama kwa sababu ya maombi."
Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam juzikati, Msama alisema tamasha hilo linatarajiwa kufanyika mwezi Aprili mwaka huu kwa tarehe itakayopangwa na baadaye litasambaa katika mikoa mingine ya Tanzania Bara.
Msama alisema: "Kwa ujumla maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea vizuri na tunawakaribisha wadhamini mbalimbali kuja kutuunga mkono ili kufanikisha tamasha hili kubwa ambalo ni maalum kuombea uchaguzi mkuu ufanyike kwa amani, upendo na utulivu."
Msama aliendelea kusema kuwa, kwa sasa jambo linaloendelea ni kuzungumza na wafadhili na wadhamini nchini ili kuweza kukamilisha shughuli hiyo.
Alisema: "Kama tukifanikiwa kuwapata wadhamini basi tamasha letu litakuwa halina kiingilio. Watu wote bila kujali imani zao wataingia bure."
Msama alimaliza kwa kusema: "Tamasha hili pia litawakutanisha waimbaji wa nyimbo za Injili mbalimbali maarufu wa Tanzania na nje ya Tanzania."