DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Mchungaji Samweli Karao wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Ngaramtoni mkoani Arusha, ameendesha maombi maalum Julai 23, 2025 kwa ajili ya viongozi wa CHADEMA, akimjumuisha Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Tundu Lissu.
Katika maombi hayo, Mchungaji Karao alimuomba Mwenyezimungu ampe Lissu wepesi wa kutoka kizuizini, huku akituma salamu maalum kwa kiongozi huyo ambaye kwa sasa yuko gerezani. Akizungumza mbele ya waumini na viongozi wa CHADEMA mchungaji huyo alimtaka Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA kufikisha salamu zake kwa Lissu, huku akitamka kwa imani maneno haya: "Neema ya Mungu imfunike." Maombi hayo yalifanyika mara baada ya ibada ya kuvunja tanga kufuatia maziko ya aliyekuwa Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Arumeru, Albert Elias Mollel.