Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,284
Ewe mwana wa zinaa, litege sikio lako,
Ibilisi kakuzaa, kahaba mzazi wako,
Umekuja na balaa, utushushie wenzako,
Timamu awa kichaa, asama vitendo vyako,
Fisi ulaye mifupa, ukivuwa ulovaa.
Si kondoo wewe fisi, hiyo ngozi ukivuwa,
Nyoka kuzaa mjusi, haiwi haitakuwa,
Ulichotaka nafasi, ufanye unoyajuwa,
Si mengine ni maasi, wasopembe kuonewa.
Fisi ulaye mifupa, ukivuwa ulovaa.
Wavaa kanzu nyeupe, usemwe msafi sana,
Ukweli leo nikupe, kiumbe wajulikana,
Una udugu na kupe, hili huwezi likana,
Leo wapi tuitupe, ma'na nafuu ya jana,
Fisi ulaye mifupa, ukivua ulovaa.
Mua kwako mkongojo, njiani wautumia,
Nakshi zake ni za pojo, si bure watutania,
Mambo yende arijojo, njaa ikakuvamia,
Tautafuna kwa fujo, tumboni utautia,
Fisi ulaye mifupa, ukivuwa ulovaa.
Hekima iko kushoto, huwezi kunibishia,
Vipi ufanye utoto, unapo badili gia,
Ukiwa uko na mato, kila pembe ya dunia,
Zege lataka kokoto, ndipo lipate timia,
Fisi ulaye mifupa, ukivuwa ulovaa.
Uchwara wako mchomo, sihofu kukueleza,
Kusema mumo kwa mumo, siwezi na sitaweza,
Ama nifunge mdomo, kwa kuchelea gereza,
Hapa mwisho wangu somo, ya leo nimemaliza,
Fisi ulaye mifupa, ukivuwa ulovaa.
Dotto Rangimoto Chamchua.(Njano5)
Call/whatsp 0622845394 Morogoro.