Mchina anyongwa ndani ya gari Dar!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,800
34,189
085A9790.jpg
Polisi wakichukua mwili wa marehemu kwa ajili ya uchunguzi.





Stori: Makongoro Oging’, UWAZI
Mfanyabiashara raia wa China aliyetambulika kwa jina la Luo Dongpeng (32), maiti yake imekutwa ndani ya gari lenye namba za usajili T145 DFY Machi 28, mwaka huu maeneo ya Kijitonyama, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar,Uwazi linakupasha.

1-10.jpg


Gari aina ya Nissan X-Trial alimokutwa amenyongwa mchina huyo.


Taarifa zilizopatikana kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo wanaoishi maeneo aliyokutwa Mchina huyo zinaeleza kuwa, gari la marehemu huyo walianza kuliona hapo tangu alfajiri ya siku hiyo lakini kadiri muda ulivyokuwa ukienda ndivyo walivyozidi kulitilia shaka maana hakukuwa na mtu aliyetoka ama kuingia.

Waliendelea kusema kwamba ilipofika saa 10.00 jioni walilazimika kulisogelea na kuchungulia ndani ndipo walipomuona mtu akiwa amelala kiti cha nyuma, walipomwamsha hakuamka wala kujigeuza ndipo waliwaarifu polisi wa Kituo cha Mabatini Kijitonyama.
085A9757.jpg



Moja ya msumali uliokuwa umetegwa kwenye gari hilo.


Mashuhuda hao walidai kuwa huenda Mchini huyo aliuawa kisha kutelekezwa na gari lake maeneo hayo kwani alikuwa na michubuko mikononi na shingoni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Alphonce Fuime alipohojiwa na gazeti hili wiki iliyopita ofisini kwake alikiri kutokea kwa mauaji hayo.

8-3.jpg


Mashuhuda wakiwa kwenye tukio hilo.


“Huyu marehemu inaonekana alikuwa akitoka casino na uchunguzi wa awali unaonesha aliuawa sehemu nyingine na akutupwa hapo.Tunaendelea na uchunguzi kuwasaka watu aliokuwa nao casino kwa mara ya mwisho,” alisema Kamanda Fuime aliyefafanua kuwa mwili huo ulipelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.Chanzo.GBP
 
Huenda walitega msumari ili endapo kungetokea vurumai wakati wa mauaji hiyo gari isitumike kuwafukuzia kwa maana ingepata pancha
 

Hayo mauaji yanaashiria ni mageni hapa nchini, so huenda kuna uwezekano mkubwa kapigwa loba na wenzake wamedhulumiana huko cassino. Ukipata habari kuhusu hili tukio endelea kutujuza kama wakikamatwa etc. Hii kwangu ni interesting murder case.
 
Wachina ni nadra sana hapa Tz kutembea mmoja mmoja, huyo atakuwa kauawa na wachina wenzake au wamemlengeshea
 
Back
Top Bottom