Mchezo wa Yanga SC na Simba SC, Hamdan Said afungiwa miezi 3 kwa shambulizi la Dube na Kassim Mpanga afungiwa miezi 6 kwa Goli la Simba

Mchezo wa Yanga SC na Simba SC, Hamdan Said afungiwa miezi 3 kwa shambulizi la Dube na Kassim Mpanga afungiwa miezi 6 kwa Goli la Simba

Mawele

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
352
Reaction score
1,036
1772800877967.png

Mwamuzi Msaidizi namba mbili katika mchezo wa Yanga SC na Simba SC, Hamdan Said amemfungiwa miezi mitatu kwa kosa la kusimamisha shambulizi la mchezaji Prince Dube dhidi ya Simba dakika ya 61, akidai alikuwa eneo la kuotea.

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu imesema baada ya kufanya tathmini imebaini Dube hakuwa katika eneo la kuotea.

Aidha, Mwamuzi Msaidizi namba moja wa mchezo kati ya Yanga SC na Simba SC, Kassim Mpanga amefungiwa miezi sita kwa kukataa goli la Simba.Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu imesema baada ya tathmini imebaini hakukuwa na kosa kabla ya kufungwa kwa goli hilo.
TAARIFA KUTOKA BODI YA LIGI KUU TANZANIA@ligikuu @tanfootball @championshiptz @firstleague_tz@n.webp

TAARIFA KUTOKA BODI YA LIGI KUU TANZANIA@ligikuu @tanfootball @championshiptz @firstleague_tz...webp

Lakini waamuzi nao wasiwe mambumbumbu wa kujitetea kwani hao wataalam tajwa waliotafsri hizo Sheria,si wamezitafsri hizo Sheria baada ya kwenda kuangalia upya video za matukio?je kwa muktadha huo mwamuzi/msaidizi hiyo room ya kuangalia upya video akiwa eneo la tukio ndani ya sekunde 3 anaipata wapi?kwani zile VAR tulizooneshwa msimu ulioisha kabla haujaanza(mwezi wa 6-2024)ziko wapi ili nawao wawe wanafanya review kabla ya kuadhibiwa.
 
Lakini kumbe pamoja na Simba kufanya yote hayo yaliyotajwa kwenye adhabu lakini bado mmeshindwa kushinda,means bila hivyo yanga angeshinda kiulaini.YANGA BINGWA tena
 
Wame balance maamuzi hakuna kitu hapo zaidi ya kuweka VAR kwenye hizi mechi wameletewa VAR bure kabisa wao wamezifungia Temeke mpaka utasikia hazipo huku mechi zikichezwa bila VAR mnakuja kuwaonea marefa bure maana mechi zinachezwa kwa kasi sana mnaoamua mpo kwenye viti mkirudisha video za Azam ambazo sidhani kama zinakua kwenye angle sahihi ya kila matukio..
 
Kipa wa Dodo,a jiji na ushirikina wote aliofanya hajafungiwa, adhabu ya kufungiwa mechi tatu ya Selemani Mwalimu ni yakujitakia kwani tayari wachezaji wawili wa Simba walishafungiwa kwa makosa yanayofanana na hayo lakini yeye anafanya kosa la kujirudia
 
Sasa kwa tech yetu tunayotumia, viwanja na kiasi cha malipo sio kwamba waamuzi wataisha kwa kufungiwa?
 
TFF wana uchungu wa kukosa mapato hasira zao wanaitoza faini Simba.
 
Back
Top Bottom