Mchezo uliochezwa na Serikali na makampuni ya simu juu ya makato ya miamala ya simu

eng.kwenyula

Member
Jan 3, 2016
40
24
*KILICHOFANYWA NA SERIKALI NA MAKAMPUNI YA SIMU KWENYE MAKATO YA MIAMALA YA SIMU NI KALE KAMCHEZO KA' KAMPA KAMPA TENA.*

Ndugu zangu kama mlikuwa hamjua ni kwamba haya malumbano kati ya serikali na makampuni ya simu juu ya hili zigo la makato ya 28% ( 18%VAT +10% UShuru) limlemee nani! kumbe watwana wanatuhadaa!! Walishafanya yao kitambo.

Ipo hivi, toka mwezi June kipindi serikali inajadili juu ya hili zigo la ongezeko la mapato kule gizani Dodoma tayari zigo lilishamlemea mnyonge yaani mimi na wewe na Makampuni kama ambavyo Serikali imeagiza hivi karibuni.

============$$=========

Kabla ya mwezi June ulikuwa ukitoa pesa tigo pesa kuanzia 200,000/=Tsh hadi 299,999/=Tsh ulikuwa unakatwa 3,500/=Tsh

Lakini mwezi June hadi sasa makato yameongezeka kwa 28.57%
Ipo hivi,
Ukitoa kuanzi 200,000/=Tsh hadi 299,999/=Tsh unakatwa 4,500/=Tsh.

Imetoka 3,500/=Tsh hadi 4,500/=Tsh.

Ukitafuta asilimia ya ongezeko.

((4,500 - 3,500)/3,500) x 100% = 28.571428571 %

~ 28.57%.

Huo ndio ukweli wadau. Serikali yetu inatufanyia usanii tuu huku ukweli wanaujua.

Leo nimetoa pesa iese roho imeniuma sana lakini nikajipa moyo na kale kamsemo ka! IFM redio. *"HUU MCHEZO HAUHITAJI HASIRA"*

Unaweza kujiridhisha na attached documents.
=======================

By Eng. Shaaban Kwenyula
 

Attachments

  • 1467663598888.jpg
    1467663598888.jpg
    64.5 KB · Views: 50
  • 1467663610493.jpg
    1467663610493.jpg
    56.3 KB · Views: 51
aiseee...!! Ijumaa iliyopita nilitoa 290,000/= hela waliyonikata sikuamini macho yangu.
 
Shida iko wapi mbona huwa unahonger ata 20000/= kwa night moja ,lipa kodi acha kulialia
Lakini mheshimiwa raisi aliahidi atafuta makoddi ya "hovyohovyo" ila hapa mfanyakazi ndo anaonja joto ya jiwe, huku aliahidi kabisa anafahamu maisha ya watumishi kwa sababu ye mwenyewe alishapitia huko sasa mbona mambo yanakuwa kinyume? Nimekatishwa tamaa Sana na huyu jamaa. Ngoja niendelee kumpa mda labda hali mambo yaweza kuwa sawa.
 
Lakini mheshimiwa raisi aliahidi atafuta makoddi ya "hovyohovyo" ila hapa mfanyakazi ndo anaonja joto ya jiwe, huku aliahidi kabisa anafahamu maisha ya watumishi kwa sababu ye mwenyewe alishapitia huko sasa mbona mambo yanakuwa kinyume? Nimekatishwa tamaa Sana na huyu jamaa. Ngoja niendelee kumpa mda labda hali mambo yaweza kuwa sawa.

Sikiliza kijana makamuni ya cm yamekuwa yakiongeza ada za kutoa fedha kimya kimya ,lakini tumekuwa hatusemi ,na hiyo hela wala haitunufaishi, na serikali wala haipati kitu , benk hivyo hivyo ,mfano bank zilikuwa zinakata 300, wakaja 500, 800..1000 kote huko hatukupiga kelele ,leo ghafla tunapiga kelele ,kwa kuwa seikali inataka imapte kodi ,
Na kwenye miamala ndio chanzo kizuri cha kodi wala sio kodi za hovyo hovyo
 
Shida iko wapi mbona huwa unahonger ata 20000/= kwa night moja ,lipa kodi acha kulialia
Wewe unalipiwa utaonaje shida!? Shida tunaona sisi tunaolipa wenyyewe. We endelea kusifu na kutukuza .
 
  • Thanks
Reactions: 999
Kuna benki moja nao kwenye ATM zao wamebandika matangazo ya gharama mpya za matumizi ya mashine hizo kuanzia June 24 au June 23 mwaka huu.
 
Watakaoisoma namba ni hao masikini walioichagua CCM.

Matajiri hawana habari na hayo makato.
 
... na bado natakiwa kumfikisha kileleni mwanamke....
"Kuzaliwa mwanaume..." RIP TX Moshi
 
  • Thanks
Reactions: 999
Back
Top Bottom