The Zanzibar Echo
JF-Expert Member
- Apr 21, 2025
- 490
- 836
Maafisa wa uhamiaji wa Marekani wamemkamata mshambuliaji maarufu wa ndondi wa Mexico Julio Cesar Chavez Jr, mwenye umri wa miaka 39, na wana mpango wa kumrejesha Mexico ambako ana "kibali cha kukamatwa... kwa kuhusika kwake katika uhalifu uliopangwa", maafisa wa Marekani wametangaza Alhamisi.
Chini ya wiki moja kabla ya kukamatwa kwake, mwanandondi huyo bingwa wa zamani wa uzani wa kati alishindwa na mchezaji wa ndondi Jake Paul katika mashindano yaliyofanyika huko California.
Maafisa wa Marekani wanasema ana uhusiano na kundi la dawa za kulevya la Sinaloa la Mexico lakini wakili wake alikataa madai hayo.
"Chini ya Rais Trump, hakuna aliye juu ya sheria - ikiwa ni pamoja na wanariadha maarufu duniani," msemaji wa Idara ya Usalama wa Nchi (DHS) alisema katika taarifa kufuatia kukamatwa kwake.Wiki mbili kabla ya pambano dhidi ya Paul, Chavez Jr alifanya mazoezi ya hadhara huko LA ambapo alizungumza na LA Times juu ya kuongezeka kwa uvamizi wa wahamiaji ambao umelikumba jiji hilo katika mwezi uliopita.
Alisema kuwa mkufunzi wake mwenyewe alihofia kuja kazini, kwa sababu ya kuogopa kufukuzwa.
"Mimi ninatoka Sinaloa, ambako mambo ni mabaya sana, na kuja hapa, katika nchi nzuri yenye kila kitu... na kuona Trump akiwashambulia wahamiaji, Wahispania, bila sababu. Kutokuwa na Mungu kunakufanya ufikiri unajua kila kitu. Trump alifanya uamuzi mbaya."
Aliongeza: "Baada ya kila kitu kilichotokea, nisingependa kufukuzwa.