Mchawi wa UKAWA ni UKAWA wenyewe

Mchawi wa UKAWA ni UKAWA wenyewe

Kilaza

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2013
Posts
3,324
Reaction score
1,378
Mchawi wa UKAWA ni UKAWA wenyewe!!

Kwanza nianze kwa kuwatakia mafanikio mema na ushindi wa kishindo rafiki zangu wote vijana ambao wameonesha nia ya kuwatumikia watanzania kwenye uongozi katika ngazi mbalimbali ninawaombea mpate kibali hicho na mimi mungu akipenda nitaungana na nyie muda ukifika!

Lakini pia ni muda mrefu sasa sijaandika hapa labda kwasababu ya uvivu au sikuona umuhimu wa kufanya hivyo!

Baada ya maneno hayo machache turudi kwenye mada katika tafakuri iliyopita nilisema "...Sioni upinzani ukiingia Ikulu mwaka huu kwasababu CCM inategemea kura za wajinga na idadi ya wajinga ni kubwa kuliko idadi ya wanaojielewa..."

Nikaendelea kusema ".....maeneo yenye wajinga wengi ndio ngome kuu za ccm mfano Kati ya shule 10 zilizofanya vibaya kidato cha nne 7 zinatoka Tanga mkoa ambao ndio ngome kuu ya CCM huku maeneo ambayo angalau mtoto anafika kidato cha nne kama Kilimanjaro sioni CCM ikishinda labda upareni huko kwenye Njaa..."

Msimamo wangu haujabadilika hata kidogo na umebaki uleule CCM itashinda urais lakini itapoteza majimbo mengi !!

Lakini sasa neno "Mengi" kwenye majimbo nimeanza kulitiliashaka Mashaka yangu ni baada ya ccm kubadilisha Mgombea sote tulikuwa tunajua Lowassa ndio mwenye asilimia kubwa ya kupeperusha bendera ya CCM huku ikitabiriwa kuwa Slaa ndio atakaye peperusha bendera ya UKAWA hivyo watu wengi walikuwa wanategemea Lowassa atamvaa Dr. Slaa nilikuwa sina tatizo juu ya uwezo wa Dr. Slaa kupambana na Lowassa ungekuwa ni uchaguzi kati ya ufisadi na uadilifu lakini sasa baada ya CCM kubadilisha uelekeo wa Tsunami iliyokuwa inaelekea upande wao nakuanza kushambulia kutokea Mashariki ya mbali nimeanza kupata mashaka tena mashaka kwelikweli lakini mashaka haya ya mjinga yakiangaliwa kwa jicho la tatu yanaweza kutoa mwanga!

Kama wapinzani tunakibarua kizito mbele yetu siku zote mziki unapobalika hata staili ya kucheza inapaswa kubadilika ccm wameshabadilisha mziki na kumuweka mtu wanayedhani kuwa anajua staili ya mziki unaopigwa ni either upinzani ubadili mtu na kumuweka mtu anayejua vyema staili ya mziki unaopigwa au wakumbuke staili ya mziki wakati mziki umeisha.

Kwenye siasa hakuna kitu kibaya kama kutabirika yaani unakua umemrahisishia adui yako kazi na anajua vyema ni semehu gani za kupiga Kila mtanzania anajua Dr. Slaa atasimama kugombea Urais kupitia ukawa na kama sio yeye basi kwa mbaliiiiii Lipumba atabeba jahazi CCM wamejipanga kushambulia tena hasahasa kumshambulia Dr. Slaa kama ambavyo upinzani ulikuwa umepanga kumsulubu Lowassa na kwa mbaliiii Membe akipitishwa na CCM lakini CCM hawajakubali kutabirika wamefanya turudi nyuma tukajipange upya wakati huo tunajipanga wao wanasonga mbele.

Ningekua mshauri wa CHADEMA/UKAWA ningeshauri haya

1) Jumanne tusimtangaze mgombea urais kupitia UKAWA bali tungetangaza kukipa mamlaka cCHADEMA kutoa mgombea urais Hivyo mchakato wa kutafuta mgombea urais ungeanza ndani ya CHADEMA.

2) Mchakato wa kuchukua fomu ungeanza mara moja watu kama Dr. Slaa, Tundu Lissu, Prof. Baregu, Prof. Safari Nk wangeombwa kuchukua fomu huku kurugenzi ya habari kama ina watu makini (Japo siamini hivyo) wangehakikisha upepo unabadilika kwenye vyombo vya habari kama magazeti na TV na kwenye mitandao ya kijamii na hata vijiweni na kuwa ni habari za CHADEMA kusimamisha mgombea urais kwa niaba ya UKAWA.

3) Baraza Kuu lingeitwa kuchagua mgombea urais japo mikutano ya baraza hilo ichukue siku 4 na kurushwa moja kwa moja na channel kama 4 hivi ili habari nchi nzima iwe ni moja tu nani atapambana na Magufuli?

Kwa maoni yangu ya kijinga mtu anayeweza kucheza huu mziki na Magufuli ni TUNDU LISSU tena ukizingatia Lissu ni "Talk of the town" kwasasa kama ilivyokuwa Slaa 2010 hii itawafanya CCM warudi kutafuta silaha za kupambana na Lissu na kutuacha tusonge mbele! ! wakirudi watatukuta tuko mbali mno Magufuli anazo skendo kibao zakumchapa kiulaini kama tutamuweka mtu sahihi ambaye ni Lissu Mchawi wa UKAWA ni UKAWA wenyewe either waingie kwenye uchaguzi huu na mtu sahihi au walazimishe waumie vibaya.

Kuendelea kuamini Dr. Slaa ataleta upinzani mkubwa kuliko ule wa 2010 ni mahaba ya kiwango cha juu kabisa yaliyoziba uwezo wa akili kutafakari vizuri.

Lipumba na Slaa wote wagombee ubunge.

Narudia tena huu ni mtazamo wa mjinga and I stand to be corrected.
 
Good analysis indeed. Ila hapo kwa Tundu lisu naona abakie kwenye ubunge mchango wake ni muhimu sana bungeni na kwa taifa. Watafte mbadala mwingine kwa sasa
 
Hakuna mtu anayeweza kumpa urais semi-kichaa
labda lisu ajaye siyo huyu ninayemfahamu wasasa. in short he is behaving like childish.
labda Prof. Beregu au Prof Safari, hapo sawa. hata huyo slaa asahau urais. tukutane octoba.
 
No hata magufuli ni mchapakazi mzuri lakini akiwa chini ya mtu.dr slaa mvuto wake umekwisha
 
Kweli Chadema machizi Yaani unamlinganisha prof Lipumba na hivyo vitaka TAKA Vya Chadema? Kweli ukawa hapa hakuna.
 
Mkuu, ingawa sikubaliani na wewe kwa asilimia 100%, lakini kwa mbaliiii sana UKWELI NDANI YA BANDIKO LAKO. KWA KWELI MHE: TUNDU LISSU ANAUWEZI WA KUMDHIBITI MHE: MAGUFULI KWA HOJA. Sijui umefunuliwa na nani kuhusu kaukweli haka. Tujitafakari.
 
Niwazo zuri, lakini watakubali? au unataka kuanzisha ugomvi ndani ya Chadema? unataka umtamanishe na kumwaminisha Tundu Lisu yamkute ya Zitto?
 
Hili wazo la kuwaachia CHADEMA watafute mgombea ndani ya siku nne hata kama watamrudisha huyo huyo Dr Slaa ni wazo murua. Cc Tumaini Makene afikishe haraka sana wazo hili
 
Last edited by a moderator:
mtoa mada mawazo yako ni mazuri mno,kiasi kwamba ndo mjadala huku mitaani kwetu.mtu wa kumweza magufuri ni Lisu tu.ubarikiwe mkuu kwa idea nzuri,umenifanya nitoe mchango wangu leo.
 
Wazo zur ...ila Nina Wazo endapo LISU ana umaarufu kama wa Dr Slaa 2010 Je hatuon kuwa matokeo yatakuwa kama Yale aliyopata Slaa 2010?
 
Mimi binafsi sikubaliani na Tundu Lisu kutoka bungeni wakati kuna mengi ya kufanya bungeni. kuna suala la katiba mpya, kuna kutunga sheria zinazotokana na katiba mpya, kuna kupitia upya mikataba ya awali. Akiwa atashindwa ktk urais akawa nje ya system tutapoteza. Kwenye urais akae mtu ambaye hata akikosa urais madhara bungeni yawe kiduchu.
 
Mimi binafsi sikubaliani na Tundu Lisu kutoka bungeni wakati kuna mengi ya kufanya bungeni. kuna suala la katiba mpya, kuna kutunga sheria zinazotokana na katiba mpya, kuna kupitia upya mikataba ya awali. Akiwa atashindwa ktk urais akawa nje ya system tutapoteza. Kwenye urais akae mtu ambaye hata akikosa urais madhara bungeni yawe kiduchu.

hapo umenena.
 
ukawa wataendelea kuisikia na kuichungulia ikulu kwa zaidi ya miaka 10 tena
 
Back
Top Bottom