sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,685
- 1,111
Naunga mkono vita dhidi ya rasilimali zetu ambazo tumezinadi wenyewe kupitia mikataba ya siri ya kisultani Mangungo iliyofanywa na CCM yenyewe ,na leo takribani miaka 17 toka kukabidhi rasilimali madini kwa wakoloni leo ndiyo wanajifanya kushtuka.
Miaka 17 hiyo ya mateso na kupaza sauti kwa baadhi ya Watanzania walioonekana wachochezi na wanafiki kuzuia urasimishaji madini yetu kwa wakoloni wa kisasa,hatimaye leo juhudi zao zimeeleweka.
Ni ujinga mkubwa kukumbuka kuwa tunaibiwa ilihali Nyamongo,Resolute na kwingine kote kumebaki mashimo matupu,kiasi cha kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira,mali zimekwenda tumeachiwa synoide,sumu inayotafuna familia zetu ambazo sumu hiyo ilielekezewa kwenye vyanzo vya maji,huko Nyamongo.
Mh. Msigwa,mbunge wa Iringa mjini alipokuwa akimnukuu Albert Stein " We can't solve problems by using the same kind of thinking we used when we created them. Ndicho tunachokiishi leo hii,CCM kupitia serikali zake ilijifanya dalali wa rasilimali za taifa kwa kuingia mikataba ya kilaghai isiyo na manufaa kwa taifa leo hii wamepata wapi uchungu ilihali tumekwisha kupoteza mali nyingi kupindukia.
Wakati wapinzani wanahoji mikataba hii na uwazi wake,mh. Juma Ngasongwa aliyekuwa waziri wa mipango na ubinafsishaji alitamka wazi bungeni kuwa mikataba ni siri ya serikali, haipaswi kujadiliwa bungeni,mbaya zaidi kauli hiyo iliungwa mkono na wabunge wa CCM baada ya party caucus yao na kukizima kilio cha wapinzani,wachache waliokuwepo kipindi hicho.
Haikuishia hapo,usiri wa mikataba uliendelea kupigiwa chapuo na wanachama hao kindakindaki wa CCM(wabunge) kwa kura zao za siyoooooo,mikataba haipaswi kuletwa bungeni pale mh. Mnyika alipopeleka hoja binafsi kuhusu mikataba hiyo kujadiliwa bungeni.
Swali,uzalendo huu wa ki CCM unatoka wapi leo hii kupinga na ku sapoti kuzuia kusafirishwa kwa makinikia waliyoyauza kwa mikataba ya usiri! Ni lini basi CCM itakuwa mzalendo kwa taifa lake na kuzionea huruma rasilimali za Watanzania!?
Mwalimu JK Nyerere aliwahi kusema"mfumo gani huu,mfumo wa kishetani,kuwangang'anya ardhi walio wengi na kuwakabidhi wachache,tunapaswa kuzitumia rasilimali zetu to the maximum kwa maslahi ya nchi".
Tumeachia TANNEX kwa miaka mingi ikifanya tafiti za madini kwa kupeleka udongo Ulaya na Asia mpaka ikamaliza mikataba yake,leo tunaposimama kupinga udhalimu ulifanywa na level ile ile iliyotengeneza tatizo bila kuruhusu usiri wa mikataba kuwekwa wazi tunatafuta nini.
Watanzania kupitia mifumo iliyopo tumekuwa wabunifu wa kutengeneza deal kupitia udhaifu wa mikataba tuliyofunga kwa kusababisha migogoro isiyo na tija kwa taifa, kwa kesi zinazo kuja kuligharimu taifa kwa kulipa fidia za hasara za kubumba zenye lengo la kunufaisha kundi fulani.
Mh. Zitto Kabwe alimsihi rais mteule mapema sana mara baada ya kukabidhiwa nchi,kuipitia mikataba yote yenye maudhui kimsovero kwa kuirudisha bungeni,akiaanisha hasara kubwa taifa inayoipata kuipitia mikataba hiyo tatanishi,lakini hakuna aliyestuka,leo tunazuia tulichokubaliana na kimkatàba hatuoni hasara tunayo itafuta kulipa fidia kabla ya mikataba yenyewe kutolewa kwenye shubaka la usiri!
Sina nia mbaya na serikali, nimtake mh. Rais na serikali yake kuwasilisha rasmi mikataba bungeni ili kilichomo ndani kiwekwe bayana,ili watunga sheria waipitie upya bila ushabiki kwa maslahi ya taifa,kinga ni bora kuliko tiba,tupate kinga ya kisheria itakayo ruhusu kutokomeza mikatabaka kandamizi.