Mchawi Anahitajika Uingereza, Mshahara Tsh. Mil 105 kwa Mwaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchawi Anahitajika Uingereza, Mshahara Tsh. Mil 105 kwa Mwaka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jul 10, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Mapango ya Wookey Hole Thursday, July 09, 2009 4:18 AM Baada ya mchawi aliyekuwa akifanya kazi katika kituo cha kitalii cha Somerset nchini Uingereza kustaafu, mchawi mpya anatafutwa kuziba pengo lake na mshahara wake utakuwa takribani Tsh Milioni 105 kwa mwaka. "Hatuna mchawi hivi sasa, tunatafuta mtu wa kuziba pengo lake ambaye jukumu lake litakuwa ni kufanya mambo yote ambayo wachawi hufanya" Daniel Medley meneja wa kituo cha utalii kwenye mapango ya Wookey Hole alinukuliwa na gazeti la Daily Telegraph la Uingereza. Mchawi atakayefanikiwa kunyakua kazi hiyo atatakiwa kuishi kwenye mapango ya Wookey Hole yaliyopo Somerset akiishi na paka wengi sana huku akiwafundisha uchawi watalii watakaokuwa wakiyatembelea mapango hayo. Mchawi atakayechaguliwa atatakiwa kulifanya pango hilo lionekane kama lilivyokuwa enzi za kale ambapo mwanamke mmoja mchawi alikuwa akiishi kwenye pango hilo na inasemekana aliwaroga wakazi wa eneo na kuwaletea mabalaa ya magonjwa mbali mbali. "Jukumu la mchawi atakayechaguliwa liko wazi, Ishi kwenye pango na fanya mambo yote ambayo wachawi hupendelea kufanya" alisema Daniel Medley. Wachawi watakaojitokeza watafanyiwa majaribio julai 28 mwaka huu mbele ya timu ya majaji maalumu watakaowapima wachawi uwezo wa kufanya mambo ya kichawi na tabia zao. Medley alisema kuwa wanategemea watu wengi watajitokeza kuwania nafasi hiyo kwani mshahara wa paundi 50,000 (takribani Tsh. Milioni 105) kwa mwaka uliotangazwa ni mkubwa sana. Mtu atakayefanikiwa kunyakua kazi hiyo atakuwa bize sana na shughuli za kichawi mwishoni mwa wiki na wakati wa likizo za mashule nchini Uingereza. http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2451454&&Cat=2
   
 2. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #2
  Jul 10, 2009
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Eeebwana eeee Niko fiti mno!!!!! Ngoja nikawashangaze wazungu. Naomba unipe details vizuri. Nitawawa kilisha vema wana JF na nusu ya mshahara wangu nitatoa kwa ajili ya JF.
   
Loading...