Mchango wa wanawake katika maendeleo nchini

Mema Tanzania

Mema Tanzania

Verified Member
48
125
#KIPOPOONFRIDAY

MCHANGO WA WANAWAKE KTK MAENDELEO NCHINI
Tanzania ni sehemu ya mataifa mengi duniani ambayo yanaadhimisha siku ya wanawake duniani. Mwanamke ameendelea kuwa nguzo ya ujenzi wa uchumi nchini licha ya wengi wao kukumbwa na umaskini wa kipato (Income Poverty). Takwimu zinaonyesha wanawake wanajumuisha asilimia 52% ya taifa la kazi. Wengi wao zaidi ya 60% wamejiajiri katika shughuli za kilimo (hii ina maana zaidi ya 60% ya chakula kinachozalishwa nchini kinapitia katika mikono ya wanawake).

Pia wanawake wameendelea kwa kiasi kikubwa kuchangia pato la taifa kwa kujihusisha na shughuli za kiuchumi km ujenzi, viwanda, madini na sekta isiyo kuwa rasmi ambayo inajumuisha zaidi asilimia 80 ya ajira nchini ikiwemo mama lishe, sekta ya ujasiliamali nchini zaidi ya asilimia 54 inamilikiwa na wanawake ambao wanafanya biashara tofauti zinazosaidia kusukuma maendeleo ya familia zao na taifa kwa ujumla.

Ni ukweli usiopingika jukumu la kulea jamii humtegemea mwanamke, licha ya kuwa kazi nyingi wanazo zifanya kama kuchota maji, kupika hatuzichukulii katika kipimo cha ujenzi wa uchumi lakini zinachangia kwa kiasi kikubwa katika ustawi wa jamii na utulivu katika familia. Kwa wastani mwanamke hutumia masaa zaidi ya 6 kwa siku kufanya kazi zisizokuwa na malipo ambazo kama zigeuzwa kuwa za malipo basi zingezalisha nusu ya ajira zilizopo.

Sio kwamba wanawake wasifanye hizi kazi, ila ni lazima jamii iweze kuzithamini kazi hizi na kuhakikisha haziathiri ustawi wao kwa kuwepo na mgawanyo mzuri wa majukumu ya kifamilia. Ustawi wetu wa jamii kwa upande wa malezi na ukuaji huamuliwa na wanawake ambao tangu mtoto anapozaliwa na kukua mwanamke ndiye anayehakikisha ukuaji imara wa mtoto. Hivyo tunapojinasibu kuwepo kwa amani, usalama, furaha na nidhamu katika jamii ni matokeo ya mchango mkubwa wa mwanamke. Ni wanawake katika familia wanaohimiza watoto kwenda shule, kusimamia lishe bora kwa watoto na familia. Jukumu la wanawake ni kubwa sana katika maendeleo ya kielimu na afya katika familia na taifa kiujumla.

Siasa na uongozi imeendelea kuwa mhimili mkubwa katika kuamua maendeleo ya taifa letu. Miaka ya nyuma ilikuwa ni ngumu kwa wanawake kujiingiza katika siasa na uongozi. Tamaduni na malezi kwa kiasi kikubwa yalimuweka mwanamke kuona nafasi ya kuona siasa na uongozi ni mchezo wa wanaume.

Taratibu jamii yetu ilianza kubadilika kifikra na kuanza kuamini na kuwapa nafasi wanawake. Tumeshuhudia hivi karibuni wanawake wakithubutu kuchukua nyadhifa za kisiasa na kiungozi hali inayochangia kuingiza fikra mpya na kuleta maendeleo katika taifa letu. Taasisi na makampuni makubwa kadhaa yanongozwa na wanawake na yamekuwa yakifanya vizuri kuleta mchango wa maendeleo nchini.

Viongozi kama Mama Anna Makinda, Gertrude Mongella, Asha-Rose Migiro wamechangia kwa kiasi kikubwa kuleta maendeleo ya taifa kupitia nafasi tofauti walizozishika. Mfano, Gertrude Mongella aliongoza Mkutano wa Beijing mwaka 1995 ambao ulichangia kwa kiasi kikubwa kuasha hali ya wanawake kupigania haki zao na kuamini wanaweza kushikiriki katika shughuli za kisiasa na kiongozi.

Ukweli usiopingika wanawake wengi katika uongozi wameendelea kuwa waaminifu kimaadili maana ni mara chache kusikia mwanamke amekumbwa na kashfa za rushwa, ufisadi au uhujumu uchumi.

CHANGAMOTO WANAZOPITIA WANAWAKE
Licha ya kuchangia maendeleo kwa kiasi kikubwa,wanawake wanakumbwa na changamoto nyingi zinazoendelea kukandamiza ustawi. Changamoto ni za kiuchumi pamoja na kijamii -

Umaskini wa muda |wanawake hutumia muda mwingi kufanya kazi za nyumbani hali inayomkwamisha kujihusisha na shughuli za kiuchumi. Hutumia muda mwingi kutika kuteka maji, kusanya kuni, kusimamia familia hii inawapelekea kuwa na muda mchache wa kujiingiza ktk shughuli za kuwaingiza kipato na hii hupelekea wanawake wengi kuwa maskini wa kipato na hasa vijini ambapo mgawanyo wa majukumu ya kijinsia (Gender roles) hauna uwiano mzuri.

Changamoto za kijinsia katika elimu | Wasichana wengi uandikishwa shule za msingi kuliko wavulana. Lakini ni wachache humaliza masomo ktk elimu ya kati (O-level) kwa sababu tofauti ikiwemo mimba za utotoni, miundombinu isiyo rafiki ya hedhi salama, ndoa za utotoni na majukumu ya nyumbani.

Mgawanyo wa kipato katika kilimo | Wanawake wengi wanajihusisha na kilimo, lakini wengi wanaishi ktk umaskini wa kutupwa. Hii huchangiwa na mfumo usio rafiki katika uzalishaji na ukusanyaji mapato (Wanaume ndio huwa waamuzi)

Changamoto za ziada katika ujasiliamali | kwa wanawake inajumuisha mifumo ya kifedha na kisheria. Wanawake wengi hawakopesheki sababu hawana dhamana za kuomba mikopo kama ardhi ambayo zaidi ya aslimia 80 inahodhiwa na wanaume. Taarifa za masoko na teknolojia zinawakwamisha wanawake wengi ktk kujiingiza na kuendeleza shughuli wanazofanya za kijasiliamali.

Tamaduni juu ya majukumu ya kijinsia | Kazi zisizokuwa na malipio/kazi za nyumbani zinafanywa zaidi na wanawake, huu mtazamo ukiambatana na desturi na mitazamo ya kiimani inawakwamisha wanawake ktk kujiingiza ktk shughuli za uzalishaji mali.

Japo wanapitia changamoto zote hizi, wanawake wameendelea kuwa imara ktk kuliletea maendeleo taifa letu. Maadhimisho haya ya siku ya wanawake duniani yatazidi kutambua na kuthamini mchango wa wanawake na kuzidi kupata haki zao za msingi wanazo stahili pasipo kujali jinsia zao. Hakuna wa kuwawezesha wanawake, tayari wamesha tuonesha wanaweza, kikubwa ni kuendelea kuwaunga mkono.
 
kakamkubwa

kakamkubwa

JF-Expert Member
1,179
2,000
Wanatupikia, kuzaa watoto na kuwalea ni mambo ambayo mwanaume hamudu kwa kweli
 

Forum statistics


Threads
1,424,900

Messages
35,075,540

Members
538,137
Top Bottom