MICHANGO KWA WANA VIJIJI BAGAMOYO
Sisi ni Wakazi wa Bagamoyo tunapenda kuleta malalamiko yetu kwa Mhe. Magufuli kwamba kumeanzishwa michango ya lazi kwa kila mwanakijiji (kila kichwa) kutoa michango ya sh 10,000/ tunachojiuliza jamani sisi wenyewe hali zetu za kimaisha ni mbaya sana ni vigumu hata kupata sh 10,000 kwa mwezi halafu leo tunaambiwa tutoe michango tuwapatie Wenyeviti wa vijiji na vitongoji eti kwa ajili ya maendeleo ya vijiji ambayo kwa kweli hatujui ni yapi.
tafadhali Mkuu wa Wizaya ya Bagamoyo tunaomba fuatilia hili halafu tuelezwe ni nini kinachoendelea tunateseka na kukamatwa kwa wale ambao tumeshindwa kutoa michango hiyo hasa katika kitongoji cha Kaole. Mkuu wa Mkoa tunaomba tusaidie baba jamani twendde wapi sisi masikini jamani. kama hamuani njooni hapa Kaole mjionee wenyewe mateso haya Mhe. Magufuli tusaidie sisi wanyonge!!!!