Kibunago
JF-Expert Member
- Jan 11, 2008
- 300
- 122
Deogratias & Fatma,
Hongereni sana kwa kipindi chenu cha Hoja. Leo mmejitahidi zaidi isipokuwa wachangiaji ndio hawakuwa na hoja za nguvu sijui kwa sababu mlichukuwa Mainjinia zaidi ambao tunatania kuwa ni watu wa namba zaidi kuliko malumbano ya kifilosofia na itikadi kama wale ma Social & Political Scientists waliopita.
Anyway, naendelea kutoa ushauri kuwa mjitahidi sana kupata wachangiaji kutoka vyuo tofauti na makundi tofauti na tasnia tofauti na jinsia tofauti na fani tofauti ambazo zote zinahusika katika mada husika.
Kwa mada ijayo ihusuyo ajira, sasa pata wachangiaji kutoka Wawakilishi wa Chama cha Waajiri; Vyama huru vya Wafanyakazi, Wizara ya Elimu, Wizara ya kazi na Maendeleo ya Vijana, Vyama vya Siasa, Wanafunzi na Waalimu wa Business Studies, NGOs zinazohusiana na ajira , Mwakilishi Idara ya Uhamiaji, Mwakilishi EAC, Mwakilishi Vyombo vya habari n.k.
Na mimi Kibunago mwakilishi kutoka mitandaoni, naanza mchango wangu kwa mada ya wiki ajayo kuwa:
Watz lazima tubadili hisia, mitizamo na uwajibikaji juu ya dhana ya kazi na Uteja kwa ujumla.
Kwanza tujiamini katika ushindani wa kutafuta na kuanzisha ajira ambazo tunaweza.
Pili tupende kazi zetu tunazopewa na tuzifanye kwa moyo na bidii kwa kufuata maadili ya kazi au taaluma.
Tatu, tuendelee kumpokea Mteja kama Mfalme kwa vitendo na si kwa maneno ya kwenye mabango.
Nne, elimu itolewayo iwe ya kumwandaa mtu kuongeza ushindani katika soko la ajira la leo duniani. Yaani hata kuandika Resume nzuri na barua ya maombi na namna ya kujiandaa vyema kwa ajili ya Mahojiano na mwajiri na kufahamu Haki za Mteja n.k hayo yafundishwe sana kuanzia Sekondari.
Aidha ni vyema tuelewe kuwa ajira ya kujiajiri na ukuaji wa sekta binafsi lazima ikuzwe na kupigiwa debe sana nchini kuliko vijana kuwa wanakaa wanasubiri tu ajira ya Serikalini. Kukua kwa sekta binafsi kutaongeza tija na ushindani na uthamani wa bidhaa na huduma zitolewazo nchini na hivyo kuongeza pato la Mtz na uchumi wetu kwa ujumla.
Nawaachia wengine wajibu swali ambalo mimi sitalijibu bali haya nayaona kuwa ni muhimu katika soko la ajira.