Mchanganuo wa mikataba ya sportpesa na vilabu vya Simba SC na Yanga SC

Deadbody

JF-Expert Member
May 30, 2015
4,274
6,592
MCHANGANUOA WA MIKATABA YA SPORTPESA NA VILABU VYA SIMBA SC NA YANGA SC

YANGA

LOGO-YANGA.jpg

Mkataba wa jumla wa Yanga SC na Sportpesa ni shilingi 5,229, 349,688.

Mkataba huu una ongezeko la asilimia 5% kila mwaka lakini ongezeko hilo linaanzia mwaka wa pili wa mkataba.

Mchanganuo:
1. Mwaka wa kwanza Yanga SC watapokea shilingi 950,000,000.
2. Mwaka wa pili watapokea shilingi997, 500,000. Ikiwa ni ongezeko la asilimia 5 la shilingi950 za mwaka wa kwanza.
3. Mwaka wa tatu Yanga watapokea shilingi 1,047, 375,000.
4. Mwaka wa nne watapokea
1,099,743,750.
5. Mwaka wa tano watapokea shilingi 1,154,730,938.

SIMBA SC

Simba-The-Lion-King-Blu-Ray-simba-29326762-1209-680.jpg

Katika mkataba huu Simba SC kwa ujumla watapokea shillingi 4,862,555,500.

Mkataba huu una ongezeko la asilimia 5% kila mwaka lakini ongezeko hilo linaanzia mwaka wa pili wa mkataba.

Mchanganuo

1. Mwaka wa kwanza Simba SC watapokea shilingi shilingi 880,000,000.
2. Mwaka wa pili kukiwa na ongezeko la asilimia 5 watapokea shilingi 924,000,000.
3. Mwaka wa tatu klabu ya Simba itapokea shilingi 970,000,000.
4. Mwaka wa nne watapokea shilingi 1,018,710,000.
5. Mwaka wa tano watapata shilingi 1,069,645,500.

Tofauti kati yao ni shilingi 386,794,188/-.

Bonus kwa vilabu vyote viwili ni kama ifuatavyo .

1. Ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara ( VPL ) shilingi 100,000,000/-
2. Kagame ..........
3. CAF ...........
 
Timu zingine zina safari ndefu sana kama kila mtu anataka adhamini hawa wawili kwa madau makubwa!!
Ila ndala watagawana na timu zingine kwa kununua mechi na kununua wachezaji wajambishe!
Simba wakishinda poa, wakishinda Yanga wamenunua mechi.

Zikifungwa timu nyingine hali ya mchezo, ikifungwa Simba points zinatafutwa mezani hadi Fifa
 
Hivi kwanini hawa wadhamini awaziangalii timu ndogo ndogo kama stand,mbao,nk?hizo timu zikipata mdhamini mnono kama wa simba na yanga,watafanya vizuri sana nakuongeza ushindani mkubwa.Ebu angalieni stand utd wakati acacia wapo,walileta upinzani mkali sana.
 
Hivi hawa sportpesa ni nani haswa? Naona hadi Everton wamewaweka nyavuni.
Si wa mchezo.
 
Hujasema hao sportpesa wanafaidikaje. Kudhamini simba na Yanga ni sawa na kudhamini pooltable, timu hazina malengo ya mbali zaidi ya kukashifiana.
 
Hujasema hao sportpesa wanafaidikaje. Kudhamini simba na Yanga ni sawa na kudhamini pooltable, timu hazina malengo ya mbali zaidi ya kukashifiana.
Hao Sportpesa wanafaidika kwanza nembo yao tu kukaa mbele ya jezi ni biashara tosha kabisa,
 
Hivi kwanini hawa wadhamini awaziangalii timu ndogo ndogo kama stand,mbao,nk?hizo timu zikipata mdhamini mnono kama wa simba na yanga,watafanya vizuri sana nakuongeza ushindani mkubwa.Ebu angalieni stand utd wakati acacia wapo,walileta upinzani mkali sana.
Stand yupo pia, anakula ml 600 nazan kwa mwaka
 
Hivi kwanini hawa wadhamini awaziangalii timu ndogo ndogo kama stand,mbao,nk?hizo timu zikipata mdhamini mnono kama wa simba na yanga,watafanya vizuri sana nakuongeza ushindani mkubwa.Ebu angalieni stand utd wakati acacia wapo,walileta upinzani mkali sana.

Jibu unalo wewe mwenyewe. Lazima ujue mdhamini hatoi pesa kama hisani.
Nini kilitokea kwenye udhamini kwa Stand United? Ugomvi, uzandiki, uadui, kushikana uchawi, majungu, fitna, ulozi hadi mdhamini akaona hapa ujinga tu!

Kuna kazi kubwa ya kuutoa mpira wetu mikononi mwa wanaojiita 'watu wa mpira'. Hawa ndio vikwazo vya mabadiliko
 
Nakubaliana nawewe kabisa kwa ili.Soka la TZ linaendeshwa nawatu wenye masilahi yao binafsi.Migogoro ndani ya virabu inaibuka tu baada yakuona pesa mfano mzuri ni stand,awa jamaa walipata udhamin mnono sana na timu ikafanya vizuri.lakini kilichotokea kila MTU anajua
 
Nusu ya izo pesa Ndala watanunua mechi washangilie ubingwa feki. ........mechi za kimataifa swambulengee. ......out.
 
Back
Top Bottom