The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 5,902
- 19,093
Benki kama taasisi ya fedha mapato yake makubwa ni kutikana na huduma inazotoa kwa wateja kama vile riba ya mikopo na makato ya huduma.
Tukizungumzia hasa makato ya benki(bank charges) kwa mteja anapotoa pesa au kuhifadhi pesa au kudai kujua salio lake. Mfano kwa benki ya NMB ukiwa umejiunga na NMB mobile na ukataka kujua salio lako unakatwa TSHS. 300.
Na ukichukua pesa kwenye ATM machine unakatwa TSHS. 800. Pesa hiyo siyo yote ni faida kwa benki husika, mfano umekatwa hiyo 800 haimaanishi yote ni faida kwa benki, hapo kuna gharama za uendeshaji wa hiyo ATM mashine na gharama za kulipia hiyo mashine maana tunajua hiyo sio mali ya benki nao wamenunua toka master card au visa. Kwwnye hiyo 800 faida inaweza kua 300 ukitoa gharama za uendeshaji.
Serikali kwa kujua au kutokujua wana taka wakate 18% ya 800 yote ambayo ni Tshs 144. Ukichukua 300 ya faida ukatoa 144 ya VAT benki inabakia na faida ya 156.
Hiyo Tshs. 156 inayobaki mwisho wa mwaka inakatwa kodi ya mashirika(corporate tax 30%), maana yake 30%*156=46.8 au Tshs. 47.
Kwa kiswahili chepesi ni kwamba faida ya Tshs. 300 Inakatwa kodi mara mbili jambo ambalo sio sahihi na ni kinyume cha sheria..
Tukumbuke gharama hizo ziliwekwa na benki bila ongezeko la thamani baada ya benki kufanya tathmini zao na kuona watapata kiasi gani, leo serikali haiwezi kuja kuzilazimisha benki kua gharama hizo ambazo hazina ongezeko la thamani benki zikubali iwe ina ongezeko la thamani.
Serikali yetu iache kukurupuka na kufanya mambo na kutoa matamko ambayo hayana uhalisia.
Nyerere alikua na kilimo cha kufa na kupona, mwinyi akaja na ruksa, mkapa ukweli na uwazi, kikwete kilimo kwanza, awamu hii wamekuja na kukurupuka.(kukurupukalization)