Ndugu nakushauri nenda kaione hiyo nyumba haraka kabla ya hela. Baada ya kuikagua na kuona na dalali, panga siku uende ukiwa peke yako au na mkeo mkaongee majirani wawape historia ya hiyo nyumba (dalali asijue).
Pia ulizia kama kuna mgogoro wa kifamilia. Ukiridhika na majibu yote hayo. Fanyeni malipo kwa mashahidi, pia upewe valid docs kama hati ya makabidhiano n.k. Waweza hata kumtafuta mmiliki halali aseme kwanini anaiuza. Jiridhishe kwa 100%, ukiridhika.
Mungu akutangulie katika hili. Siku njema