Mchakato wa kubana Matumizi watua Halmashauri...

displayname

JF-Expert Member
Feb 15, 2013
1,972
1,082
Wanabody...

Baada ya kupunguzwa kwa Wizara na kuungananishwa tukiaminishwa dhana ya kupunguza/kubana matumizi sasa....upanga huo umetinga rasmi kwenye Serikali za Mitaa kwa maana ya Halmashauri, Miji na Majiji...

Matumizi yanapunguzwa kwa kuvunja baadha ya idara au vitengo visivyo na majukumu yenye tija au yanayohusiana na kwa kuunganishwa ili kupunguza...matumizi ya mishahara na malupulupu kwa waku wa idara na vitengo husika.

Mfano Idara ya Ujenzi na Maji hapo yawezekana ikawa ni idara moja chini ya Mhandisi mmoja ili zile fedha za mshahara wa scale ya LSS takribani 3M, pamoja na posho ya Nyumba, Fenicha, usafiri na mawasiliano vibakie kwa mkuu mmoja tu na si wakuu wa idara mbili kwa majukumu yanayolandana kama Elimu Msingi na Sekondari...

Mfano kitengo cha Uchaguzi...ukiisha tu ishu za kisheria kwa wapinga matokeo huratibiwa na kitengo cha Sheria hivyo hakuna haja ya kuwa na Mkuu wa Kitengo cha Uchaguzi anayelipwa mshahara wa mkuu wa kitengo na malupulupu yooote kwa kazi ya muda mfupi tu.

Ndio adhma yenyewe hiyo.... kubana matumizi na kufunga mkandaa na kuvuuuta soksi zetu juuu.

Hofu yangu:-
Wazo ni zuri ila...kwa walioongeza miaka ya kustaafu na wanahivyo vyeo leo ila kesho vikaota mbawa na kupaa..hatma ya pensheni zao zitakuwaje?! Kwa maana mshahara atakao staafia bila shaka utashuka..

Magonjwa ya ghafula sambamba na vifo... hii yaweza ikawa ni matokeo ya kuchukua mkopo kwa mshahara wa Milioni 3 kisha leo warudishwa chini mshahara...makato yake na takehome yaweza leta shida kwa afya za waahanga husika.

Sina hakika na route za kwenda kuagua kama zitaongezeka au lah.

Att: mfano wa mapendekezo hayo
1465799592713.jpg

Ikumbuke kuwa kila serikali za mtaa zimeambiwa zipendekeze zenyewe kabla ya TAMISEMI kutoa uelekeo wao wa muundo MPYA wa kubana matumizi utakaoanza mapena an bajeti mpya hapo Julai mosi.

Karibuni kwa mjadala huru.

Displayname.
 
Back
Top Bottom