Mchakato wa Katiba Mpya

jogoolashamba

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
348
195
Kuondoka kwa Mwalimu Nyerere kumeacha Tanzania bila matumaini! Watu wazima lakini hawaoni/hawajui hata wanalolifanya. Mmeng'ang'ania kukusanya mawazo ya wanavijiji kuhusu Katiba mpya wakati hata jina la nchi yenyewe bado liko mashakani. Itaitwa Tanzania, Shirikisho la Tanganyika na Zanzibar au Katiba itakuwa ni ya Tanganyika? (Wazanzibari wana yao)! Haya sukumeni twende, kwa sababu hata matatizo wenzetu huyaita mafanikio!
 

Chibolo

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
3,985
2,000
Inaonekana hufuatilii mchakato mzima ndo maana unaleta pumba hapa jamvini! Cjui umetoka wapi!
 

jogoolashamba

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
348
195
Inaonekana hufuatilii mchakato mzima ndo maana unaleta pumba hapa jamvini! Cjui umetoka wapi!
Chibolo acha upinzani usiokuwa na elimu wala tija! Au kumtaja Nyerere ndiyo kumekuchafua, najua wengine mna chuki binafsi na mzee yule. Hata unakotokea sasa naweza nika"guess".

Wote tunajua mnaendesha mjadala wa Katiba ndani ya Muungano, lakini hakuna anayeusema muungano ndani ya Katiba Mpya kuogopa kufa ghafla kama ilivyotokea kwa Prof Chachaghe. Historia ya wenye akili wote........"Thinkers".........inabainisha Muungano ungejadiliwa kwanza ili kipengere cha Kwanza kitamke nchi inayohusika. Sheni anataka Serikali 2 Makmu wake anataka Shirikisho.....Wakubwa hawa! Utawalazimisha serikali 3 wewe na CHADEMA yako? Au utatumia ujasusi manake linchi lote limegeuka genge la majasusi!
 

jogoolashamba

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
348
195
Inaonekana hufuatilii mchakato mzima ndo maana unaleta pumba hapa jamvini! Cjui umetoka wapi!
Come on up Chibolo! Are u one of those who fight anonymous battles on the net? Nitakutilia shaka kuwa ni typical case ya Wabongo wanaopiga kelele za "Simba na Yanga" kama wasomi kweli kweli! Lakini ukiwakurupusha na hoja za mambo makubwa zaidi wanatoa matusi kama "bunduki ya rashasha" ili usijue kama hawaelewi unalolisema. Jina la Chibolo tu limenishtua kwa sababu ndiyo matusi wanayotumia kama silaha ya kujihami kutokana na Ujinga, au mseniiii....ge. Wepesi sana kwa lugha hiyo. Generali Defao mpaka leo hapandi jukwaani kutumbuiza kwa sababu ya wabongo bwana, kwa matusi tu.

Tuanzie hapo basi....Wewe una jamvi ambalo unataka tulitumie kwa makini! Ok! Sema kama mchakato wa Katiba ukikamilika 2014 wakati Wazanzibar hawajaamua aina ya Muungano wetu utaweza kuiandika Katiba yako? kwa nchi ipi? Hayo siyo maswali yanayoweza kujibiwa na wakulima vijijini!
 

MpendaTz

JF-Expert Member
May 15, 2009
1,721
1,250
Jogoolashamba ukweli utasimama na kubakia ukweli hata watu waukatae vipi. Hakuna mfano mwingine wa muungano kama wa wetu hapa duniani. Na kwa kusema hivyo ni baada ya pia kutillia maanani kuwa si lazima tuige ila kama uliopo unaonekana ni ubunifu wa hasara kwa pande zote na hauna mantiki tena basi sidhani ni busara kuendelea kuyakumbatia makosa badala ya kuyasahihisha.
Swala la Katiba mpya ya Tanzania kuandaliwa kabla ya kurekebisha kero za Muungano na kurekebisha muungano wenyewe ukae sawa na uwe na manufaa kwa pande zote ni kucheza kamari gizani. Msomi yeyote anayeelewa maana ya muungano hilo lazima alione. Kinachonishangaza na nadhani tupo wengi, ni kitu gani kilichoachwa huko kwenye hizi Ikulu na itikadi za hiki chama tawala ambacho kinafanya viongozi waogope kulishughulikia jambo hili kwa umakini unaostahili? fumbo gani lipo hapo? Kitu gani kinachosababisha hata kutoana roho kwa ajili ya hili jambo?
 
Top Bottom