Mch. Christopher Mtikila (RIP),Tanzania itakukumbuka hasa wakati huu

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,137
17,908
Ungekuwepo,ungeshafanya jambo kimahakama. Ungesha-uchallenge ubabe na ubatili unaoendelea na kulalamikiwa nchini kwasasa. Nilikuwa nakujua. Usingekaa kimya. Ungethubutu. Tuliobaki hadi tunatia aibu. Waoga watupu. Hata ID zetu ni za bandia,za uogauoga.

Kweli ulikuwa Baba wa Katiba wa Tanzania. Ulikuwa ni mtanzania jasiri kuliko wote. Usingebaki nyuma. Kutazama amri zikizidi sheria. Kutazama aliyehifadhi akisemwa ameficha. Ungetusaidia. RIP Comrade!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Ruvuma)
 
Je, Serikali ikiagiza sukari itahiifafadhi wapi? au itaificha wapi? Ole wenu serikali mkiagiza sukari muifiche. Tunataka iwekwe uwanja wa Taifa au Karume au Mnazi mmoja. Uwiiiiiiiii ngachoka mieee
 
Namkubali sana Mtikila alikuwa hawezi kutunza unafiki. Nakumbuka alivyokosoa uamuzi wa CHADEMA kumchukua Lowassa na baada ya hapo kupata ajili tatanishi iliyokomesha maisha yake hapa duniani.
 
Je, Serikali ikiagiza sukari itahiifafadhi wapi? au itaificha wapi? Ole wenu serikali mkiagiza sukari muifiche. Tunataka iwekwe uwanja wa Taifa au Karume au Mnazi mmoja. Uwiiiiiiiii ngachoka mieee
Ndo maana serikali yenyewe inawatupia mzigo wa kuagiza wafanyabiashara, wanaogopa kijitumbua wenyewe. Itabidi waagize tu ili sisi wanachi tuwe watumbuaji
 
Sahihisho

Rev. Mtikila(RIP) Hakua baba wa katiba ya Tanzania. Alikua baba wa katiba ya Tanganyika. Na ndio kitu pekee nilikubaliana nae. Alikua mtanganyika halisi. Rest in Peace
 
Mungu hawezi kukutoa duniani kama bado hujamaliza kazi aliotarajia uifanye. vinginevyo uwe umekiuka wito. ukaenda jjia zako
 
Back
Top Bottom