MCC jitafakarini upya na majigambo yenu ya bure

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,380
MCC JITAFAKARINI UPYA NA MAJIGAMBO YENU YA BURE.

Kwanza na mimi leo nijitokeze sio kukosoa bali kujengana kwa uwazi na ukweli juu ya Wafadhili hawa MCC na wale wengine takribani 10 waliojitoa kuifadhili nchi yetu tanzania.

Kwanza niwapongeze kwa woga wa kujitoa kufadhili(inferiority of the Impact), pili mtajisalimisha wenyewe baada ya kujiona mlichofanya ni maharage ya mbeya yaani soya.

Kwa muda mrefu sana Nchi zinazoendelea zimekuwa zikinyonywa na mataifa makubwa yaliyoendelea kwa kigezo cha ufadhili na wanapowafadhili wengine hutaka fadhila hata ya kumiliki migodi au rasilimali fulani eti kwa kuwa tu wanafadhili nchi husika. Na mkiwanyima chochote hawawapi ufadhilli, nacho hisi mimi ni kuwa katika maandishi inaonekana wanafadhili kweli lakini katika maneno huenda nao wanafadhiliwa kwa kupewa fadhila ya kishika uchumba(rasilimali).

Nchi yoyote duniani inakuwa nchi bora pale inapoweza kubuni vyanzo vya mapato na pia kusimamia vizuri ulipaji na upokeaji wa kodi kama chanzo cha kuanza KUJITEGEMEA. Nchi inajitegemea hasa ikikusanya kodi vizuri na kwa kufanya hivyo inafikia nchi husika haihitaji msaada wowote kutoka kwa hisani au wafadhili na ikihitaji basi ni kidogo tu hasa pale penye mkwamo.

Mataifa makubwa yanapoona nchi imeshajitambua kwa kukusanya kodi vizuri huchukia maana ulaji wao unapotea, hivyo huanza kutoa visingizio kama tunajitoa kufadhili ikiwa ni njia ya kukimbia aibu itakayowapata. Unashangaa wanajitoa na nchi inasonga mbele tu.

Mnakumbuka sakata la ESCROW hawa MCC hawakusema wanajitoa? na leo wanasingizia chanzo ni uchaguzi Zanzibar wakati lile la Escrow halisemwi tena? sasa wanajitoa kwa lipi lile la Escrow au la Zanzibar au kuna jingine tusilolijua?

Wao wajitoe salaama lakini watarudi kupiga magoti wakisema Tanzania badilisheni utaratibu, natamka leo, kesho kutwa watakuja na jingine.....mdororororororororororoooooooo.

Mwandishi wa Kimakala hiki ni Mwalimu katika Jiji la Mwanza;

Deogratius Nalimi. I. Kisandu/Deogratius Pio Kisandu
Mtumishi Mdogo Sana wa Mungu.
4/4/2016
 
Back
Top Bottom