Mbwembwe za muungano, nini maana yake?

Maarifa

JF-Expert Member
Nov 23, 2006
4,568
2,911
Wapenzi wana jamvi wa jamii forums!! ninawasalim katika jina la Tanganyika
maonesho ya jana ama hakika yameniacha na maswali mengi sana.; ingawa yalipendeza sana na kutuhakikishia ulinzi imara na kwelikweli!!!
1. sijawahi kuona maandalizi ya kijeshi kwa shughuli ya kushrehekea uhuru wa Tanganyika ama muungano kama mwaka huuu. Madege yalikuwa yakivurumushwa Dar, zanzibar, Dodoma , pemba n,k. KWA NINI?

2. Siku ya Siku ( Jana ) pamoja na mbwembe nyingi Majeshi (Yalionesha hadharani what capable they are. masilaha mazito mazito, miavuli, anga , majini mpaka na komandoo- kupasua tofali vichwani!! So what?

3. wakaalikwa marais wote jirani - Malawi- mgongoro wa nyasa umefikia wapi? ,, Kagame- mwakilishi alikuwepo- kuna fukuto, ethiopia, kenya, uganda, burundi, zambia , msumbiji, na wakongwe wapigania uhuru wengi-

je Kikwete alitaka kupeleka mesage gani? kwa majirani, kwa wanaoonekana kuupinga muungano???????
fedha kiasi gani zilitumika kuwaleta wote hao- walialikwa wakalipiwa first class air tickets na wasaidizi wao na wakafikia five star hotels!! duhh hiyo budget ingefanya nini katikia vituo vya afya? madarasa?
 
Hizikuwa ni salam kwa wanao taka serikali 3, na wale wanao ichokonoa nchi yetu, muungano utalindwa kwa garama zozote zile, ulikuwa hujui hata hlo?
 
IC kweli sasa naamini hilo. maana wananchi wengi wana maoni tofauti.je utaulinda kwa Madege na kupasua vigae kichwani? mie hapo tu ndo shida yangu!! nafikiri Muungano ungelindwa kwa njia ingine kuufanya uwe mzuri na bila KERO!!
 
Hata wazazi wako walipo funga ndoa walifanya sherehe kubwa sana kulinganisha na uwezo wao.
 
Hata wao wanafanya hivyohivyo, hukuona kule korea kaskazini nchi inayoendeshwa kisiri sana lakini tuliona mikombora ikipita mbele ya wananchi. Member wengi fb tunao imekuwa shida sana.
 
Mkuu Maarifa mimi nachelea kusema kuwa yawezekana ni amri toka kwa Amiri Jeshi Mkuu either kwa lengo la kunogesha sikukuu, kupeleka ujumbe kwa majirani, kufikisha ujumbe kwa UKAWA au yeye binafsi anapendezwa na maonesho ya kijeshi.
Nimesema yawezekana ni amri toka juu kwa sababu katika uongozi wa maraisi watatu waliopita hatukuwahi kuona maonesho ya hivi japo resources (madege, faru, komandoo, fedha) zote zilikuwepo.
Kama lengo ni kuonesha uimara wa jeshi letu hapo sidhani kama tutakuwa sahii kwani wenzetu hatujui wako imara kiasi kipi na kama ni kujihami kuulinda muungano pia hatutakuwa sahihi kwani muungano ni wa wananchi ili wafaidi mali zilizo ndani ya nchi ilhali jeshi linatakiwa kuimarisha mipaka ili wananchi wasiingiliwe.
Kikubwa ninachojiuliza ni kuwa, Je jeshi linafanya vitu hivi kwa kupenda au linalazimishwa?
 
Last edited by a moderator:
Ni akili ndogo inayoongoza akili kubwa, huku mc wa jeshi akilopoka anachotaka mpaka akanza jishtukia, hii nchi ipo pabaya sana baba liz anajaribu udikteta
 
Hata wazazi wako walipo funga ndoa walifanya sherehe kubwa sana kulinganisha na uwezo wao.

Kwa hiyo tumefanya jubilee ya miaka 50 ya kumuoa mke wetu Zanzibar kwa gharama kubwa sio?
 
Mleta mada hata mie nimejiuliza sana kwani haikuwahi kutokea sherehe tena za muungano kuonyesha vifaa vingi hivi vya kijeshi! Halafu nilikuwa naangalia sura za hawa wageni waalikwa, they were very serious! Hawakuwa wanacheka hata kidogo especially m7 na jamaa freedom! nadhani kuna meseji flani walikuwa wanaisoma! Siyo bure kuna kitu zaidi ya tuyajuayo just time will tell! Anyway labda Malawi, Rwanda & co. walikuwa wanapewa ujumbe kwani hata kauli ya siku zote ya mkulu ya ''watakao tuchokoza watakiona cha mtema kuni'', hata mc wa jeshi naye aliirudia!
Pia waalikwa walikuwa wengi mno, dah zaidi hata ya sikukuu zingine! Kuonyesha siraha nyingi kama hizi nilidhani ni sahihi tu kwenye sherehe za uhuru ama za majeshi! Otherwise, they were purposely terrifying somebody!
 
Hizikuwa ni salam kwa wanao taka serikali 3, na wale wanao ichokonoa nchi yetu, muungano utalindwa kwa garama zozote zile, ulikuwa hujui hata hlo?

Mambo ya serikali 3 si yako bungeni na pia yanajadiliwa na wananchi katika mchakato ea kupata katiba mpya.? Tangu lini mchakato wa kupata katiba ukawa kosa na tishio mpaka misuli ya jeshi itunishwe kwa wananchi?
 
IC kweli sasa naamini hilo. maana wananchi wengi wana maoni tofauti.je utaulinda kwa Madege na kupasua vigae kichwani? mie hapo tu ndo shida yangu!! nafikiri Muungano ungelindwa kwa njia ingine kuufanya uwe mzuri na bila KERO!!
Hao wanaopasua tofari kwenye kichwa mbona mmoja M23 waliweza kumuua kile DRC? hayo ni mazingaombwe tunapokuja kwenye uhalisia hao wote hawatasaidia chochote kwani bila kushirikiana na sisi wananchi hilo jeshi si lolote
 
Serikali ya Tanzania inakaribia kuwekewa vikwazo na UN kwa kubreach mikataba. Korea Kaskazini imewekewa vikwazo ila nchi hii imejiingiza kudeal nao kwa kuchukua wataalamu wa mafunzo ya kijeshi wako Mwanza wakiwafundisha JWTZ ugereji wa army hardwares
 
Back
Top Bottom