Mbwembwe za kaka yangu

Mbwembwe za kaka yangu

Kashaijabutege

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2010
Posts
2,696
Reaction score
740
Siku moja fundi wa simu alitumwa na bosi wake kwenda kwa Advocate Rutakyamirwa. Ruta alipomuona fundi akanyanyua simu ya mezani na kuanza kuongea kwa mbwembwe.

How are you Kajumulo? Vipi Chicago? Sisi tuko fine, ila mwanangu Rwejuna ndiye aliibwa TZS 1bn za matumizi alipokuwa akiogelea beach. Bahati nzuri 2bn zilizokuwa kwenye mfuko wa suruali hawakuziona.

Mie nitafika huko next week kwa ajili ya kumtetea Obama kwenye kesi ya defamation. Of course, i will come with wife and our last born. Can you believe kwamba Obama namtetea bure?...

Baada ya kuona Ruta haachi maongezi, yule fundi akamshitua na kumwambia Bosi, kwaheri. Ruta kusikia hivyo, akaweka receiver chini na kuuliza "what is your problem kijana"?

Yule kijana akamjibu, nimetumwa na Bosi wangu kuja kukuunganishia hiyo simu yako ya mezani. Lakini naona umeshaanza kuitumia, inawezekana Bosi wangu kakosea kunituma hapa.

Ruta kwa mapomp na kusevu soo akamwambia fundi " Let me take out my wireless device so that you could continue". Akajifanya anachomoa "device" na kisha akamruhusu fundi aendelee.

Mjini hapa.
 
Hawajamaa bana, full masifa, na karibu wote kutoka ule mkoa ndo walivyo
 
hata mimi naona,ila ni wakali hao ukiwaambia
 
Back
Top Bottom