Dereva wa magari makubwa Mwana-mama aliamua kutafuta mbwa wa kumlinda ajapo safarini. Akampata mbwa kwa watu wanaofundisha na kuuza mbwa. Muuza mbwa alimwambia mama, "Mbwa huyu hapendi wanaume." Mama akafurahi sana bila kuelewa nini maana ya usemi huo. Basi, yule mama akalipa pesa na kumchukua mbwa yule moja kwa moja ndani ya gari. Aliposafiri mwendo mrefu akaamua kupumzika mahali. Akiwa chini na mbwa wake wamesimama, wanaume 2 wakawa wanamsogelea pale aliposimama. Mama huyo akajua sasa ndio wakati wa kujua ni jinsi gani mbwa huyo angedhihirisha tabia yake ya kutowapenda wanaume. Ni kweli yule mbwa hakuwapenda wanaume kwani alikimbia na kujificha chini ya uvungu wa gari!!