Mbunge wangu Mwigulu Nchemba, mbona umepoa sana?

Toka aambiwe na mzee wa kuteleza ulimi "kaa chini popo we! Unadhani sijui unayogizani?" Basi hana raha kabisa. Ule ubabe wake wa enzi zile kwisha kabisa. Hata wizara sasa inasimamiwa na Bashite kiaina yeye kaachiwa kiti tu pale wizarani.
Umaarufu wa kuchonga ni shida sana, akitokea mmakonde mwingine akachonga kinyago kingine watu wataangalia hiki kinyago cha mwisho.
Pia ili kutulizwa zaidi kaletewa kitila mkumbo ili 2020 wapambane unajua kijana anautaka uraisi sasa asije leta chokochoko baadae
 
Majuzi katika lile baraza ambalo tunaapa tusitoe siri zake. Na la pili ni ndio.
Pole yake ila niliambiwa kuwa mkulu anatafuta sababu za kumtumbua ila hazipati sasa kwanini aishi Kama mtumwa??
 
Shark
Wewe ndiyo umepigilia msumali wa mwisho!

Chakaza shukrani kwa kutufungua macho ila Shark umetuonyesha njia.

Kama Kitila Mkumbo atakuja Iramba na kushinda Ubunge hiyo 2020,basi iwapo 2025 JPM akiondoka,jimbo la hili ni lazima litaenda CHADEMA.

Mwigulu ana influence kubwa kisiasa,ambayo Kitila anaikosa
 
Binafsi sijauona uwezo wa wale vijana wote waliotaka wapewe ticket ya kugombea urais kupitia CCM hapa namzungumzia Mwigu na Janu.

Wote wamepwaya, wote hakuna aliye creative, wote wameonekana kutokuwa na jipya kwenye sehemu wanazoziongoza kiasi kwamba inanipa mashaka iwapo wangeweza kuongoza vema kwa kuongezewa majukumu.

Pengine hali ya kubebana kwenye vyama ndo iliwafikisha huko na si juhudi zao. Nani anaweza angalau kututajia mafanikia yao kwenye maeneo wanayosimamia? Mmoja hali ya usalama ndo imekuwa mbaya zaidi na hana majibu zaidi ya kutoa majibu ya kisiasa. Alipo Saa8 hana majibu, waliomteka Roma hawajui, waliompiga Lissu bado anawatafuta, wengine wameamua kuwapiga raia Ukonga yeye yupo tu. Mwingine anataka viwanda vijengwe wakati mchakato wa EIA ukiendelea. Inashangaza sana. Je iwapo EIA itaonesha eneo husika halifai kujengwa kiwanda hicho nani atamlipa mwekezaji ili abomoe na kujenga kwingine. Huko si kutafuta migogoro isiyoisha toka awamu moja mpaka nyingine. Hatuwezi kujenga viwanda kwa expenses za kuharibu au kuchafua mazingira au kuwaletea wakazi usumbufu na iwapo vitajengwa maeneo yasiyoruhusiwa.

Sitashangaa wao wakirudi tena kuomba nafasi hiyo na bado wengine wakawaamini na kuwapigia chapuo.
 
Chona
Miye nadhani,ni kwa kuwa wamewa vitengo ambavyo "vinawaficha kisiasa" na hivyo kuwakosesa fursa ya kushine kisiasa.
Pia wamepewa wizara ambazo zina changamoto nyingi,hasa ile ya Nchemba kiasi kwamba,inapelekea kumchafua kisiasa.

La mwisho nadhani itakuwa ni ajenda ya JPM yakujaribu kuwafifisha,na kuwavunja moyo wasije utumia Urais wake kama jukwaa la Mwigulu na Janu kujijengamo.
 
MAPUMA MIYOGA
Mimi ni Mnyiramba upande wa mama,na nimezaliwa Unyirambani

Nawajua fika wajomba zangu nyie,kwani hiyo damu yenu inatitirika pia mishipani mwangu
 
Back
Top Bottom