Mbunge wangu Mwigulu Nchemba, mbona umepoa sana?

ChamaDola

JF-Expert Member
Dec 23, 2016
3,432
2,804
Kunani huko Serikalini?
Kulikoni Madelu?
What have they done to you?

Awamu hii imekufifisha sana tofauti na ile ya JK. Tena kuna wakati natamani urudi Chamani uachane na shughuli za kiserikali. Umepoza, hakuna shamrashamra uwapo luningani au katika majukumu yako kama miaka ile ya 2010 kwenda 2015.

Vipi? Wizara yako ndiyo inayoongoza kwa ukwiukwaji wa haki za raia na hata mauaji,mfano mzuri ukiwa na haya mashambulizi ya FFU dhidi ya raia hapo Ukonga. Wanakuhujumu au ni uzembe wako?

Wewe ni jembe, Alfayo na yule mke wa Kafulila hapa Iramba wanakufahamu fika ujuzi wako wa medani na jinsi ulivyowakata kata funua 2015 wakakosa hata kata moja.

Ebu rudi nyumbani, udi Iramba tufanye kazi
Ila swali langu bado liko palepale:
WAMEKUFANYA NINI MPAKA UMEPOA HIVYO?
 
Toka aambiwe na mzee wa kuteleza ulimi "kaa chini popo we! Unadhani sijui unayo gizani?" Basi hana raha kabisa.

Ule ubabe wake wa enzi zile kwisha kabisa. Hata wizara sasa inasimamiwa na Bashite kiaina yeye kaachiwa kiti tu pale wizarani.

Umaarufu wa kuchonga ni shida sana, akitokea mmakonde mwingine akachonga kinyago kingine watu wataangalia hiki kinyago cha mwisho.
 
Toka aambiwe na mzee wa kuteleza ulimi "kaa chini popo we! Unadhani sijui unayogizani?" Basi hana raha kabisa. Ule ubabe wake wa enzi zile kwisha kabisa. Hata wizara sasa inasimamiwa na Bashite kiaina yeye kaachiwa kiti tu pale wizarani.
Umaarufu wa kuchonga ni shida sana, akitokea mmakonde mwingine akachonga kinyago kingine watu wataangalia hiki kinyago cha mwisho.
Hiyo ilitokea kipind gani??Huyo wakuteleza ulimi ni mkulu au??
 
Chakaza

Kisa cha kuambiwa hivyo ni nini?

Kama hautojali,waweza niambie aliambiwa lini?

Kazi ipo.
Wenzake ndani ya (...na sitatoa siri za ....) wanasema mzee wa kuchakachua mastori alimuona madelu kanyoosha kidole kutaka kuchangia jambo, basi ndio hapo wote waliposhikwa na butwaa kumsikia mzee anasema maneno hayo. Madelu alisikia kudhalilika sana na kama sio visasi vya mzee kwamba ukijiuzulu ana wewe! Basi madelu angesharudi zake kufanya kazi na Wanyiramba wenzake kwa heshima kuliko ilivyo sasa. Kuna mambo mazito humo ndani! We acha tuu!
 
Huyu jamaa naona kama amepwaya mno katika nafasi aliyopo, sijui ni uwezo wake mdogo au amedhibitiwa. Nina hakika Kimoja katika hilo ni sahihi.

Pamoja na yote hayo, hivi mkiwa kwenye siasa huwezi kumjulia hali ya Afya jirani na au ndugu yako! Ameshindwa hata kwenda kumuona jirani yake, mbunge mwenzake kutoka mkoa mmoja huko aliko lazwa anaendeleaje!

Viongozi wa miaka hii ni kiboko.!!!
 
Pamoja na kuwa mie na madelu hatuivi, lakini ukweli ni kuwa hajahusika hata kidogo, kwanza siku hizi Madelu ni outsider katika mikakati michafu hawawezi kumshirikisha. Labda hiyo albadiri ya matendo ya zamani akiwa Naibu KM


Wacha kutetea wauwaji wewe jamaa anaona hadi aibu kwenda kumsalimia lissu kumbuka wote ni wabunge wa singida lazima anajua mchongo tu.


Swissme
 
Hawezi kuwatumikia mabwana wawili....ngoja amtumikie boss wake kwanza...nyie mtamwaona 2020
 
Wacha kutetea wauwaji wewe jamaa anaona hadi aibu kwenda kumsalimia lissu kumbuka wote ni wabunge wa singida lazima anajua mchongo tu.


Swissme
Kutokwenda kumsalimia Lissu sio sababu ya uhusika wake kwa tendo lile, elewa kuwa ccm wasio majasiri wote wametishwa na kile kitendo cha mwenyekiti wao kusema kumuona Lema jela ni usaliti. Tunao marafiki wengi wabunge wa ccm na baadhi ya mawaziri na wana tueleza wazi hali ilivyo huko.
Kuujua mchongo muovu hakumfanyi yeye Madelu kuwa kahusika, anaweza kuujua mchongo huo kama sisi tunavyo ujua maana sio siri tena. Madelu ameshiriki hujuma nyingi sana dhidi ya Chadema, lakini sio sahihi hata tukio ambalo hakushirikishwa sisi tumshirikishe kwa vile tuu hatumpendi. Huko kutakuwa kupotosha maana na sio haki.
 
Back
Top Bottom