Mbunge: Wanafunzi Zanzibar wapewe upendeleo...

Mbunge: Wanafunzi Zanzibar wapewe upendeleo...

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803

ALHAMISI, APRILI 25, 2013 07:22 NA DEBORA SANJA, DODOMA

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imesema kukosekana kwa wanafunzi kutoka Zanzibar wanaopata ufadhili wa kusoma nje ya nchi kunatokana na kutokukidhi vigezo vinavyohitajika.

Taarifa hiyo ilitolewa bungeni jana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, wakati akijibu swali la Mbunge wa Gando, Khalifa Suleiman Khalifa (CUF).

Katika swali lake alitaka kuwepo na mgawanyo wa nafasi kutoka Zanzibar za wanafunzi wanaopata ufadhili wa kusoma nje ya nchi badala ya kufuata vigezo ili kuepuka wanafunzo kutoka Zanzibar kukosa nafasi.

Dk Kawambwa alisema hakuna utaratibu wa kutenga nafasi maalum kutoka Zanzibar kwa nafasi za ufadhili, bali nafasi hizo hutengwa katika sekta nyingine kama vile ajira.

“Katika kuchagua wanafunzi wanaoomba ufadhili kamati huchukua wajumbe kutoka bara na visiwani ambayo huamua nani apate ufadhili na kutokana na vigezo hivyo, wakati mwingine wote walioomba wanaweza wakakosa,” alisema Dk Kawambwa.

Awali akijibu swali la msingi la Arfi, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, alisema nafasi zinazotolewa za kusoma nje ni kwa ajili ya wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisema wananchi wote wanaoomba wanashindanishwa kwa vigezo vya kitaaluma na si vinginevyo.

“Katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2012 nchi ambazo zimekuwa zikitupatia nafasi za masomo nje ya nchi ni Cuba, Algeria, Urusi, Msumbiji, Serbia, Uingereza, Misri, Korea ya Kusini, Macedonia, Uturuki, China, Ujerumani na Oman,” alisema.

Katika swali lake la msingi, Arfi alitaka kujua vijana waliopata ufadhili wa kusoma nje katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2012 na nchi walizokwenda.

 
wanataka kila kitu wawekewe nafasi zao bila kushindanishwa na wabara.. dah kweli wabara noumer wanakaba mpaka kwenye usahili na wanzanzibar wameogopa kweli kweli nakuona wanaonewa.
 
Naona anahamisha ile sera ya wanawake wakiwezeshwa wanaweze to wazinzibar wakiwezeshwa wanaweza, waombe kuwa na bunge la viti maalumu ijulikane kabisa.
 
Naona anahamisha ile sera ya wanawake wakiwezeshwa wanaweze to wazinzibar wakiwezeshwa wanaweza, waombe kuwa na bunge la viti maalumu ijulikane kabisa.
Huwezi kuwa muislamu na usiwe mlalamishi wa kipuuzi puuzi kama wazanzibar?Wao waende Omani kwa mkoloni wao si naskia wanataka kuvunja muungano ili wamrudishe aje awabake dada zao wapate watoto weupe au hawa sio wenyewe waliomuua padri kwamba kanisa ndo limeleta Muuungano kupiti Padri Karume na Askofu Nyerere???Poor Zanzibaries....Serukamba nyie
 
Mbona wazanzibar walalamishi na waropokaji kama Mwiguli
 
Back
Top Bottom