Mbunge wa Madaba Joseph Mhagama awaasa waandishi wa habari

Mar 23, 2012
64
13
WAANDISHI WA HABARI RUVUMA WAASWA NA STEPHANO MANGO, MADABA

MBUNGE wa Jimbo jipya la Madaba mkoani Ruvuma, Joseph Mhagama amewataka Waandishi wa habari katika mkoa huo, kusaidia kutangaza na kuandika fursa mbalimbali zilizopo katika halmashauri hiyo hatua ambayo itasaidia kuvutia watu wengi, kwenda kuwekeza katika jimbo la Madaba.

Akizungumza na gazeti hili jana jimboni kwake Mhagama amewahimiza waandishi kuandika habari nzuri zinazohamasisha wananchi kujikita katika shughuli za maendeleo hususani kwa zile zinazofanywa na wakazi wa jimbo hilo, badala ya kuandika au kutangaza habari za migogoro kwani zinaweza kuhatarisha na kuharibu mahusiano yaliyopo kati ya wananchi na serikali yao.

Mhagama ameungana na wadau wengi katika mkoa wa Ruvuma, kupongeza mchango mkubwa unaofanywa na waandishi wa habari hapa Ruvuma, kuandika habari sahihi na zinazohamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za kimaendeleo.

Alisema kuwa, vyombo vya habari vikitumika vizuri vina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi hapa nchini, lakini iwapo vitatumika vibaya vinaweza kuleta matatizo makubwa kama vile kuibuka kwa mifarakano kati ya wananchi na serikali yao.

Pia alieleza kuwa amewataka wakazi wa jimbo hilo kuangalia namna wanavyoweza kutumia fursa zilizopo, ili kujiletea maendeleo yao badala ya kukaa na kusubiri kuona watu kutoka nje wakinufaika na rasilimali hizo, jambo ambalo halipendezi na kwamba amewataka wakulima kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara na kuahidi kuwa serikali itajitahidi kuwa karibu nao katika suala la pembejeo za kilimo na kutoa ushauri wa kilimo cha kisasa, ili kiwe na tija kwao kwa manufaa ya kizazi cha sasa na baadaye.
 
Back
Top Bottom