Mbunge wa Kiharu, Ndindi Nyoro, ametangaza kuondoka katika chama cha United Democratic Alliance (UDA) na kujiunga na People’s Party of Kenya (PPK), hatua inayoongeza msisimko wa kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027.
Nyoro amesema yeye pamoja na wafuasi wake wameamua kuingia katika kambi ya upinzani, akidai kuwa uamuzi huo umechochewa na haja ya kutafuta mwelekeo mpya wa kisiasa. Aidha, amewataka Wakenya kuichukulia PPK kama chaguo muhimu kuelekea uchaguzi ujao.
Mbunge huyo pia amesema amekuwa akifanya mashauriano na viongozi mbalimbali wa kisiasa, akiwemo Martha Karua, James Orengo, Kalonzo Musyoka, Rigathi Gachagua na Fred Matiang’i, kuhusu mustakabali wa siasa nchini.
Hatua ya Nyoro inajiri wakati ambapo vyama vya kisiasa vinaanza kujiandaa kwa uchaguzi wa 2027, huku viongozi wakitafuta washirika na kuunda miungano mipya.
Kuondoka kwake UDA pia kunafuatia hatua ya Mbunge wa Gatundu Kusini, Gabriel Kagombe, ambaye naye ametangaza kujiondoa katika chama hicho.