Chademakwanza
JF-Expert Member
- Jun 11, 2014
- 6,346
- 1,873
Kwa taarifa za uhakika nilizopewa na mjumbe wa halmashauri kuu ya ccm wilaya,( jina linahifadhiwa)
Amesema mwisho wa Mbunge huyo ni mwaka huu. Akitembelea na kuzungumza na viongozi wa kata zote, akianza na kata 13, alikumbana na maswali mengi mojawapo ni suala la ufisadi wa Escrow na mahusiano yake na Rugemalira.
Aidha walienda mbali zaidi kwa kuhoji,ahadi za maji,barabara,umeme,mitandao ya simu na shule zote ziko katika hali mbaya.
Aidha walimhoji juu ya shule yake kwa kuwa hakuna binti anayetoka jimbo hilo aliyepewa nafasi kusoma hapo badala yake ni watoto wa vigogo tu.
Akijitetea ameahidi kuwa baada ya uchaguzi atahakikisha anatatua kero hizo.
Cha ajabu aliahidi kutoa mchango wa milioni moja kila tawi ili chama kijijenge na kuboresha ofisi za chama.
Lakini wanachama hao wamesema....alikuwa mkuu wa shirika la Maakazi duniani,alikuwa mwalimu chuo kikuu, watoto wake wanaisho nje ya nchi,amekuwa waziri wa nyumba na maendeleo,lakini ameshindwa hata kuonyesha mfano wa kutoa master plan ya mji wa Muleba......
Mama mmoja alipoulizwa alisema"...tumechoka kuburuzwa,tutaonana ndani ya sanduku la kura,tutakula kwake lakini tutalala kwingine......"
Tunachojiuliza,kwa nini fedha zitolewe sasa,wakati tunakaribia kuanza kampeni?, au ndio Escrow tena ya Muleba?