Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 36,981
- 45,903
Mhula uliopita alitoa sababu za kushindwa kwake kutimiza ahadi kadhaa kwa wananchi kua, kesi yake ya ubunge iliyokua ikimkabili, pamoja na halmashauri kua chini na uongozi wa ccm kua ni vikwazo kwake.
Alienda mbali kwa kusema kua ubunge wake ulikua wa miaka miwili tu, hivyo muda ulikua mdogo na pia ili kuweza kuweka mikakati ya jiji sawa anahitaji kuisimamia halmashauri kwa asilimia zote.
Sasa visingizio vimekwisha, sidhani kama kuna kesi yoyote mahakamani kupinga ubunge wake pia, halmashauri ipi chini ya chadema kwa asilimia zote.
Jambo linaloumiza licha ya hayo yote kutokea, ni hali mbaya ya uchumi wa jiji la Arusha, sekta ya utalii imepeta misuko suko mikubwa, wadau wa utalii wamekosa ajira, wanakaa vijiweni tu, ukipita stand ndogo ya zamani pale utawakuta magaidi wa utalii wanapiga soga tu ajira hakuna.
Mzunguko wa pesa katika shughuli za kiuchumi ni mdogo sana Arusha ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo huyu ndugu hakua mbunge wa jimbo la Arusha.
Sasa visingizio zimekwisha, tunahitaji kuona maendeleo katika jiji letu pendwa na sio siasa za kudanganyana, hatutachelewa kusikia ukisema kua umeshindwa kuleta maendeleo kwa kua wewe sio Rais hivyo tukupe urais ili utuletee maendeleo, hapo hatutakusamehe kwa kweli, na wana Arusha wanahitaji kuamka na kuacha kufanya siasa za kishabiki zinazoligharimu jiji letu na kulididimiza kiuchumi kila leo.