Mbunge unaposema jimbo langu, UMELIZAA wewe?!!

MovingForward

JF-Expert Member
Nov 10, 2009
489
49
Sipendi na ninapinga mawazo ya wabunge kujimirikisha majimbo utadhani wameyazaa wao.
Mbunge anaposema kuna watu wanazunguka zunguka katika jimbo langu, ni upuuzi!. Anatakiwa aseme kuna watu wanazunguka katika jimbo la wananchi wa MFULUKUTO!. Wanaposema jimbo langu, wanawapiga vita ya kisaikolojia watu wengine wanaotaka kugombea ubunge wawe na uoga kna kwamba wao ndiyo wanakubalika na wananchi!.

Unasema jimbo lako; umelizaa? Mke wako alibeba mimba ya miezi tisa kulizaa jimbo la wananchi!. Acheni lugha za kuwanyanyasa wananchi. Hii ni dharau! Hivi jimbo unaloliwakilisha kama Mbunge unaweza kusema ni la kwako!!. Mbunge ni mwakilishi wa wananchi, kwa lugha nyingine ni kama mshenga au agent, ambaye amepewa dhamana ya kufanya uwakilishi wa jimbo la wananchi, akiwepo na yeye mwenyewe. Ndiyo, si ni mwananchi naye wa eneo analoliwakilisha?.

Sasa, tunapompatia dhamana ya uwakilishi, kisha anatugeuka anaanza kusema hili ni jimbo lake, anataka kutuambia ametuzaa na kuwazaa wananchi? Ndiyo, ni lugha iliyozoeleka kusema Mh Mbunge wa MFULUKUTO, yaani mwakilishi wa jimbo hlo, lakini si kusema jimbo langu. Ni afadhali wangekuwa wanasema jimbo letu la MFULUKUTO!. Wanaanza ubinafsi hata katika namna ya kujitambulisha!. Wanapiga vita ya kisaikolojia. tangu lini Mkurugenzi wa Kampuni akajimilikisha kampuni badala ya wanahisa?

Mh Spika (Sitta), naamini utakuwa unapitia pitia mtandao huu wa JF, ninakuomba hivi: KATIKA BUNGE LIJALO, NINAKUOMBA UTUMIE KALE KA MUDA AMBAKO HUWA UNAKATUMIA KUWACHEKESHA WAHESHIMIWA WABUNGE, K.M UNAPOSEMA POLENI WATANI WETU WA YANGA KWA KICHAPO CHA JANA, KUWAELIMISHA WAHESHIMIWA HAO NAMNA NZURI YA KUJIELEZA WANAPOTAKA KUJITAMBULISHA, WASIWE WANAPIGA VITA YA KISAIKOLOJIA, WANAPOCHANGIA MISWADA BUNGENI AU MAHALI PENGINE. NI KISWAHILI TU CHENYE MANTIKI, KUTOKUSEMA JIMBO LANGU!!!.

TUAMKE!.
 
Washenzi sana hawa. Wanatumia vyeo vyao kujilimbikizia mamali tu. Bora hata tuwape ubunge watu wenye fweza zao tayari kuliko kuwapa waganga njaa.
 
message sent labda kweli ni majimbo yao kuna mmoja nikamsikia mheshimiwa spika jimbo langu linahitaji maji watu wangu wanalalamika ,nimeshika dhamana ya jimbo langu niwasaidie
Hayo maji mpaka kesho ni ndoto za alnacha
 
Nimekusoma sisimizi, unenenayo ni sawa kabisa basi nilisoma siku moja gazeti la Mwanahalisi liliandika "MAFIA NI YANGU SI YA KIMBAU-BUJI" mpaka leo najiuliza hivi huyu mbunge ni mzima au? wapi anapata nguvu ya kujinadi na kujitapa kuwa Mafia ni yake? si yeye tu kuna akina Buji wengi. huo ni ubinafisi na kamwe viumbe hao hawajui demokrasia maana yake ni nini? na kwa nini ipo.

Wakati count down ya kuelekea uchaguzi 2010 imeanza, wale wote wanaosema majimbo ni yao ni wale wasiojiamini na hawataki wengine wapenyeze hata pua zao huko kwenye hayo majimbo wanayodai ni "YAO" ila watanzania tunasema HATUDANGANYIKIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII
 
On point, kubwa zaidi inashiria fikira za 'Ruler' na siyo 'Leader'. Pamoja ya kwamba tunatarajia bunge la mwezi 12 2010 litakuwa na represenatation kubwa zaidi ya waheshimiwa wa opposition, lakini calibre bado itakuwa ni ile ile!
 
Back
Top Bottom