Mbunge: Tubomoe sanamu ya askari tuweke sanamu ya Diamond pale Posta

tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,330
4,119
Hayo ni maneno ya mbunge wa CCM, yule mtoto wa marehemu Celina Kombani. Ni haki yao CCM bunge lisionyeshwe live maana tangu nianze kufuatilia bunge sijawahi kusikia pumba kama hii!

Yaani mbunge analinganisha askari wetu waliokufa wakipigania nchi yetu na Daimond? Eti Daimond katufikisha mbali wapi huko??

Mchango gani kijamii kautoa hadi umlinganinshe na askari wetu? Kuna wanamichezo wanajenga shule, hospital na vingine kibao lakini huwez ukamlinganisha na nembo ya Taifa!

Daimond kafaidi yeye mziki wake na family yake, kama ni jamii basi ni kwa uchache wanaomfuata fuata.

Thamani ya sanamu ile hailingani na mtu yeyote maana inabeba majority ya askari wetu waliopigania nchi yetu.

Kweli CCM ni jipu kubwa kwa michango yao bungeni. Alikuwa anaongoza Lusinde kwa pumba naona sasa wameongezeka wengine. Lusinde aliwahi kusema nembo ya nyoka kwenye hela ya noti tutoe maana inawakilisha shetani ndio maana taifa halina hela!


14970b84bd00ed25b45f6740cf5b9cda.jpg
99b0d04fa81b4c56ad2fef9624e6bc2e.jpg


Huu ndio mchango wake mbunge wa kuchaguliwa! Sijui jukwaani anaongea nini. Nina wasiwasi na akili yake. Sintaongea lolote juu yake maana sijui akili yake. Asije akawa na tatizo kiakili nikamcheka nikachuma dhambi!
 
nilipoona hii post bado kidogo nikushambulie kumbe umemnukuu mtu kwa nchi nyingine historia ni somo muhimu sana inabidi wabunge baada ya kuchaguliwa wapewe mitihani ya kupima ufahamu wao jinsi wanavyoijua nchi hii ilianzia wapi na inaelekea wapi watakaoshindwa wapigwe chini
Yaani mimi niliona video ya huyo mbunge dogo nikaona kweli sasa tuna matatizo na namna vyama vyetu vya siasa vinavyochagua wagombea.....sijui wanaangalia nn wanapoamua mtu asimame kuwakilisha chama...inauma inapoona kijana anaongea upumbavu kama ule alafu jamaa yupo active sana bungeni anaropoka ropoka tu. Ili akirudi huko kwao sijui awaambie anachangia sana katika bunge
 
....Haya yatakuwa madhara ya utaratibu usiofaa wa mchujo wa wagombea nafasi. ...pia madhara ya wananchi kutokuwezeshwa kutambua namna ya kuchagua mwakilishi makini.

Wananchi wasipojiwezesha juu ya uchaguzi viongozi bora wasitegemee hilo kutoka ccn! Hii ni pamoja na kupiga kura kiongozi wanayemtaka na kuhakikisha wanasimamia ushindi wao... kwa njia zisizo subili mahakama zinazoshinikizwa na viongozi wa ccm.
 
Lazima ifike mahali CCM tukubali kuwa si kila mtoto wa Kiongozi anastahili kuwa kiongozi! Viongozi wengine wamefuga Mateja na baada wanalazimisha tuwape uongozi!

Hivi Mbunge kama huyu mtoto wa Celina Kombani kesho akisimama akasema ikulu ni kubwa mno igawanywe iwe studio akina Diamond warekodie Muziki! Ifike Mahali CCM tuone aibu!huu utaratibu wa kuwazawadia Ubunge watoto waliofiwa wazazi wao kama akina Godfrey Mgimwa, Sioi Solomon Sumari, Omary Kigoda na huyu wa Kombani.
 
Nilishasema hawa watu waliobebwa kwa sababu alikuwa mtoto Wa Fulani ni hatari kwa siasa za jamii yetu Na maendeleo yaani anataka nembo ya taifa awe diamond Mungu wangu kwa mfano akija siku akasema amemuunga mkono Cameroon sasa tuwe Na nembo ya shoga anajua humuhimu Wa wanajeshi wetu katika nchi kweli
 
Back
Top Bottom