Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Mbunge wa Gutundu kusini Moses Kuria amedai kuwa kinara wa upinzani Raila Odinga anajaribu kutumia njia za mkato kuhakikisha kwamba anaingia Ikulu.
Bwana Kuria alisema wito wa upinzani wa kutaka makabila ambayo yamewahi kutoa rais yaziachie jamii nyingine wadhifa huo, ni ishara kwamba Odinga anajaribu kutumia mbinu ya ili awe rais.
Akizungumza katika eneo la Gitugi, Kaunti ya Murang'a mbunge huyo wa Gutundu kusini alisema pendekezo la kutaka urais uzungushwe miongoni mwa jamii mbalimbali linakiuka misingi ya demokrasia.
Alisema wakenya wanachagua mtu binafsi kuwa rais na wala si kabila lake,wakizungumza katika kaunti ya migori wikendi iliyopita viongozi wa upinzani walisema watashinikiza kila jamii ipewe fursa ya mtu wao kuwa rais.
Upinzani hawajui wanachotaka walianza na usalama kisha wakaenda mkopo wa Eurobond, ufisadi na baadaye wakarukia maafisa wa IEBC na sasa wanataka kuzungushwa kwa wadhifa wa urais, alisema Kuria.
Chanzo : Taifa leo