Mbunge prof. Maghembe akataliwa hadharani na Wananchi

Mbunge prof. Maghembe akataliwa hadharani na Wananchi

Jumanne Mkota

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Posts
3,011
Reaction score
1,794
Mbunge wa jimbo la mwanga na Waziri wa maji Prof Jumanne Abdala Maghembe amekutana na adha ya kukataliwa mapema na wananchi kabla hata ya uchaguzi katika ziara zake kampeni zisizo na Baraka za Chama chake.

Adha hiyo alikutana nayo 16/02/2015 katika kitongoji cha Changalavo Kijiji cha Ngujini Kata ya Kisangara wilaya ya mwanga.

Awali ratiba yake ilikuwa ina mkutano wa hadhara wa wanakijiji ambapo pia ndipo Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya anapoishi na ndipo kitongoji alichozikwa mwana harakati na msomi mbobezi wa mambo ya Katiba Hayati Dr. Sengondo Mvungi.

Kwenye Mkutano huo ambapo itifaki ilivunjwa kikao kilifunguliwa na Mwenyekiti wa kitongoji hicho ambaye anatokea CCM huku wakimuacha Mweneykiti wa kijiji ambaye anatokea Chama cha demokrasia na maendeleo.

Wananchi hao walivumilia hilo lakn Mbunge akaanza kutoa matusi na vitisho kuwa kijiji cha ngujini kisahau kitu kinachoitwa maendeleo kwani kosa walilofanya la kuichagua chadema litawagharimu.

Mwananchi mmoja alisimama na kumwambia Mbunge kuwa walishasahauliwa siku nyingi so atembee mbele(yaani aondoke kabisa eneo hilo) na kama haamini kuwa hawamtaki eneo hilo aongeze neno lolote lolote lile linawahusu aone cha mtema kuni.

Baada ya Hali kuwa tete alishuka jukwaani na kukusanya msafara wake na kuondoka huku eneo hilo likihanikizwa na sauti za tapelii, mwongo, mwizi! yaani ilikuwa ni zomea zomea ya hatari

Hata hivyo Mbunge huyo aliendelea na ziara katika Kata ya Kirya ambapo pia CCM ni Chama cha upinzani ambapo pia alikutana na zomea zomea kiasi kwamba ameamua kuahirisha ziara hiyo.

Hapa jimboni mwanga siasa zake zimebadilika kiasi ambacho kinashangaza wengi. Wengi wa wananchi wanasubiri october 2015 na kama ccm itamsimamisha maghembe uwezekano wa Jimbo hilo kubaki CCM ni mdogo mno kuliko hata punje ya Ulezi ingawa vita itakuwa kali kati ya Joseph Tadayo kama CCM itamsimamisha na Henry Kileo, Au Dr. Ngoma wa CHADEMA.

Nawasilisha
 
Zomea zomea kwa CCM ishakuwa kawaida, kwao siyo habari za kutisha tena!!! Ukitaka kuwazomea na kuwatisha CCM jiandikishe kupiga kura, piga kura na linda kura yako. Hapo wanatishika sana, na lazima FFU wanaingilia kati.
 
mwanga hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!

mwanga kwa waziri wa maji hakuna maji,ni sheeeeeeeeeeeeedaaaaaaaaaaa
 
Zomea zomea kwa CCM ishakuwa kawaida, kwao siyo habari za kutisha tena!!! Ukitaka kuwazomea na kuwatisha CCM jiandikishe kupiga kura, piga kura na linda kura yako. Hapo wanatishika sana, na lazima FFU wanaingilia kati.
kweli mkuu ! halafu hivi kujiandikisha ni lini tena nchi nzima maana naona kimya kingi kama vile ilivyokuwa uchaguzi wa serikali za mitaa. Ukienda Halmashauri kuulizia hupati ushirikiano
 
Muhimu tuombe mambo yaende salama na tumpate kiongozi bora.
 
Kamanda Henry Kilewo atamtoa kamasi huyu gamba fisadi...
 
Mbunge wa jimbo la mwanga na Waziri wa maji Prof Jumanne Abdala Maghembe amekutana na adha ya kukataliwa mapema na wananchi kabla hata ya uchaguzi katika ziara zake kampeni zisizo na Baraka za Chama chake.

Adha hiyo alikutana nayo 16/02/2015 katika kitongoji cha Changalavo Kijiji cha Ngujini Kata ya Kisangara wilaya ya mwanga.

Awali ratiba yake ilikuwa ina mkutano wa hadhara wa wanakijiji ambapo pia ndipo Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya anapoishi na ndipo kitongoji alichozikwa mwana harakati na msomi mbobezi wa mambo ya Katiba Hayati Dr. Sengondo Mvungi.

Kwenye Mkutano huo ambapo itifaki ilivunjwa kikao kilifunguliwa na Mwenyekiti wa kitongoji hicho ambaye anatokea CCM huku wakimuacha Mweneykiti wa kijiji ambaye anatokea Chama cha demokrasia na maendeleo.

Wananchi hao walivumilia hilo lakn Mbunge akaanza kutoa matusi na vitisho kuwa kijiji cha ngujini kisahau kitu kinachoitwa maendeleo kwani kosa walilofanya la kuichagua chadema litawagharimu.

Mwananchi mmoja alisimama na kumwambia Mbunge kuwa walishasahauliwa siku nyingi so atembee mbele(yaani aondoke kabisa eneo hilo) na kama haamini kuwa hawamtaki eneo hilo aongeze neno lolote lolote lile linawahusu aone cha mtema kuni.

Baada ya Hali kuwa tete alishuka jukwaani na kukusanya msafara wake na kuondoka huku eneo hilo likihanikizwa na sauti za tapelii, mwongo, mwizi! yaani ilikuwa ni zomea zomea ya hatari

Hata hivyo Mbunge huyo aliendelea na ziara katika Kata ya Kirya ambapo pia CCM ni Chama cha upinzani ambapo pia alikutana na zomea zomea kiasi kwamba ameamua kuahirisha ziara hiyo.

Hapa jimboni mwanga siasa zake zimebadilika kiasi ambacho kinashangaza wengi. Wengi wa wananchi wanasubiri october 2015 na kama ccm itamsimamisha maghembe uwezekano wa Jimbo hilo kubaki CCM ni mdogo mno kuliko hata punje ya Ulezi ingawa vita itakuwa kali kati ya Joseph Tadayo kama CCM itamsimamisha na Henry Kileo, Au Dr. Ngoma wa CHADEMA.

Nawasilisha

Hili jimbo la Mwanga CCM hata wamsimamishe nani, hawawezi kuliokoa tena. Kama kunakosa ccm walifanya na Maghembe ni kumuacha kileo kulitawala hilo jimbo tokea 2011 dogo yupo jimboni na mzigo wake umeonekana.

Kwa cdm watangazania watakuwa wengi ila washau kuchuana na kileo kwani yupo mpaka kwa wananchi chino siyo viongozi tu wachama aliyowaweka kwa mkono wake.

Sijui maajabu gani yatokea kileo alikose hilo jimbo, wakati alipokuwa anafanya operesheni ya Door to Door man to man alionekana chizi, sasa chakula kimeiva naona walaji wanataka kuwa wengi sidhani kama Chadema watakuwa wajinga kiasi hicho waingie kwenye mitego ya ccm.

Hapo Mwanga ccm wakisikia kileo wanapagawa na hata week 3 zilizopita kulikuwa na kikao cha siri cha ulinzi na usalama ambacho viongozi waccm walienda pamoja na takukuru baada ya wazee wa ugweno kwenda kumuambia mkuu wa wilaya kuwa kipindi hiki asiposimamishwa Tadayo wanahamia Chadema wazi wazi na watapiga kampeni za chadema.

Ndipo wakapanga kuendeleza mkakati wao waliyokuwa wameuanzisha wa kuigawa chadema ukanda wa tambarare ili iwe vipande vipande kwa ukanda watambarare kama ilivyo ccm upande wa mlimani ambapo kuna matabaka mawili yaani wasangi(Maghembe) na Wagweno (Tadayo) sasa nguvu ya Kileo ipo tambarare yote ccm wameamua kumuwekea mtu anayetokea tambarare ya nyuma huku kwakoa ili agawekura za tambarare kisha arudi marekani baada ya mchongo kukamilika.

Tumekwisha waambia viongozi wa Chadema juu ya njama hizi ila wanatuona sisi ni wapuuzi na kutupuuza sasa wacha watufanyie mzaha sisi tufanye maauzi yetu wenyewe. Hatuwezi kuendelea kuona tunapuuzwa wakati ni chama kilichotuaminisha kuwa asiyefanya kazi na asile.

Kiukweli ccm wanahali mbaya mwanga licha ya kushinda vijiji vingi hapa mwanga ila ukweli wanajua kuwa chadema iliwapiga na waliwachezea rafu kwa kununua wagombea wao na viongozi wao mfano ni Kata ya lembeni hapa lembeni na kata ya Kileo kwenye vijiji vya kifaru,kituri,kivulini na barabarani ccm wanaelewa walitumia nguvu kiasi gani.

Chadema kuweni macho na Mwanga mtoto amekaa tumboni miezi karibia 9 sasa msije mkapoteza kwa dharau na kiburi.

Kati ya majimbo ambayo Chadema itachukua mchana kweupe ni Mwanga kama wakicheza karata vizuri kuliko hata majimbo ya moshi vijijini, Siha, same zote mbili.

Mwanga 2010 chadema haikufanya kampeni ila ilipata kura zaidi ya 5000 huku ccm ikifanya kampeni za nguvu na kuambulia kura elf 16.

Hivyo hivyo chadema moshi vijijini, Siha na same zote na vunjo walifanya kampeni za uhakika ila wakapigwa, sasa kama hapa Mwanga Cdm iliweza kupata hizo kura bila kampeni itakuwaje sasa kuanzia 2011 mzigo haujawahi achwa kupigwa?

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni# Uswi vaasu tuti tunamwinga mbwange wetu#uutweegho naye tangia muda wothe uwo twesika mshighe neri. Twemanje njama ya ccm vemuituka kileo, Na tiari vamuinga kesi ya kumbigha ashirafali iti aituke lakini mbwange niho ewasha moto nedho, Mghothi etikiwe mshitu teituka kindu.
 
Hivi hawa maprofessa wa kizamani wanadhani watoto(vijana) ni wajinga? sasa anaambia eti walifanya kosa kuichagua CDM,? kwahiyo maendeleo hayatakuja kwasababu wao ndio wameshika dola si ndio maana yake?

Ok,hakuna tatizo nadhani ameshaona taswira ijayo Asubiri tu octoba ndo atawajua vijana wakoje,mjinga mkubwa Li professa la kizamani na jinga tu.

Hizi zama sio kama za kwao,ni kizazi kipya we know kila kitu Mjinga mkubwa,
 
kweli mkuu ! halafu hivi kujiandikisha ni lini tena nchi nzima maana naona kimya kingi kama vile ilivyokuwa uchaguzi wa serikali za mitaa. Ukienda Halmashauri kuulizia hupati ushirikiano

NEC wametoa ratiba ya uandikishaji mkuu
 
Pamoja na kwamba nipo mbali lakini wadau wanamsubiri kwa hamu sana kule Kilomeni na atakapofika wananchi hawatajitokeza kabisaaaa.... A

,,,Mpare wa milimani,,,
 
Pamoja na kwamba nipo mbali lakini wadau wanamsubiri kwa hamu sana kule Kilomeni na atakapofika wananchi hawatajitokeza kabisaaaa.... A

,,,Mpare wa milimani,,,[/QUO

Aho wabigha hedi.. Nesimanya linetonga hii
 
Pamoja na kwamba nipo mbali lakini wadau wanamsubiri kwa hamu sana kule Kilomeni na atakapofika wananchi hawatajitokeza kabisaaaa.... A

,,,Mpare wa milimani,,,
ameshapanda akakutana na nyomi sifuri
 
Kila la heri kamanda Kileo naona wananchi wa Mwanga wamefunguka sasa wanataka mabadiliko ya kweli. Cha msingi weka nguvu katika kujiandikisha ndio itakuwa siri ya ushindi wako.
 
Zomea zomea kwa CCM ishakuwa kawaida, kwao siyo habari za kutisha tena!!! Ukitaka kuwazomea na kuwatisha CCM jiandikishe kupiga kura, piga kura na linda kura yako. Hapo wanatishika sana, na lazima FFU wanaingilia kati.

umenena vizuri mkuu
 
Back
Top Bottom