barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Kumekuwa na maswali mengi juu ya ushriki wangu kwenye uzinduzi wa ugawaji madawati uliofanywa na Mh Rais, katika viwanja vya Karimjee. Naomba ieleweke kuwa mimi ni mmoja wa wajumbe wa tume ya Utumishi ya Bunge
Moja ya kazi ya hii tume ni kushugulikia masilahi ya Wabunge na watumishi wa bunge,na pia kukutana na mh Rais napobidi kwa ajili ya kuboresha masilahi ya wabunge na watumishi wa bunge,. Katika kipindi chote cha bunge la bajeti Tume pamoja na mambo mengine imekuwa ikishugulikia
1. Ofisi za wabunge , majimboni
2.samani katika ofisi za wabunge
3.mgawao wa madawati kwa wabunge kwenye majimbo yao .
4. Na mambo mengine yanayohusu utawala kwa watumishi wa bunge na wabunge.
Kwa muktadha huu nadhani nimeeleweka kwa nini nilikuwepo
Pia naomba ieleweke ninapoikosoa serikali sina ugomvi "personal" na mtu yeyote lengo na nia yangu nikuiona Tanzania inasonga mbele kwa misingi ya usawa, kuheshimiana na kufuata katiba ya nchi yetu.
Tunapotekeleza yote haya , lazima uhuru na mamlaka ya bunge yaheshimiwe na BUNGE LIWE HURU KUISIMAMAI SERIKALI.Demokrasia lazima ipanuke zaidi na uhuru wa mawazo kutoka kwa kila Mtanzania , asiwepo mtu wa kuiminya DEMOKRASIA!