Mbunge: Nitawalipua vigogo wauza unga

Mbunge: Nitawalipua vigogo wauza unga

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,963
Reaction score
166,356
SAKATA la biashara ya dawa za kulevya limeibuka upya, baada ya Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM), kusema ataanika majina ya vigogo wanaofanya biashara hiyo haramu.

Akizungumza bungeni juzi, Lugola alisema anakusudia kupeleka bungeni majina ya viongozi wa taasisi za Serikali wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya kabla ya kumalizika kwa mkutano huu wa Bunge.

Mbunge huyo pia aliwatuhumu viongozi hao wakiwemo mawaziri, kwa kuhusika na vitendo vya rushwa ama mihadarati.

Katika Bunge la tisa chini ya Spika Samuel Sitta, aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum, marehemu Amina Chifupa (CCM), aliwahi kutangaza kuwa yupo tayari kutaja hadharani watu wanaofanya biashara ya dawa za kulevya.

Amina ambaye kwa sasa ni marehemu, katika mchango wake bungeni alinukuliwa akisema. “Nitawataja hadharani kwa majina, hata kama ni mume wangu anauza dawa za kulevya nitasimama na kumtaja bila kuogopa.” Mohamed Mpitanjia aliyekuwa mume wake naye ni marehemu.

Katika kile kinachoonekana ni kufuata nyayo hizo, Lugola alisema kitendo cha viongozi wa juu serikalini kushindwa kuwataja na kuwachukulia hatua wafanyabishara hao licha ya kuwajua, ni wazi kuwa nao wanahusika.

Lugola alitoa kauli hiyo juzi, wakati akichangia Hotuba ya Makadirio ya Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu, inayoshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Katika mjadala huo, Lugola aliweka wazi msimamo wake wa kutounga mkono bajeti hiyo ya waziri mkuu, kutokana na sababu mbili, rushwa na dawa za kulevya.

“Ninawaomba wabunge wenzangu, kabla ya kumaliza mkutano huu wa Bunge nitakuja na orodha ya viongozi wa taasisi za Serikali, wanaojihusisha na madawa ya kulevya naomba mniunge mkono,” alisema.

Hata hivyo, Lugola alisema Kamishina wa Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Christopher Shekiondo, anapaswa kuwajibishwa kwani ameshindwa kazi.

Lugola alisema biashara hiyo imezongwa na rushwa na kwamba hiyo ndiyo sababu inayomfanya Shekiondo ashindwe kuwakamata watu hao, licha ya kuwafahamu kwa majina.

“Kwa nini Shekiondo anatuambia anajua majina ya watu wanaofanya biashara ya kulevya, lakini hatutajii eti kwa kuwa wanashindwa jinsi ya kuwakamata.

“Hakuna cha kushindwa hapa kama sio rushwa nini, awajibishwe kama anashindwa kuwakamata, kwanini kama kuwakamata ni tatizo wasiombe msaada hata kwa FBI kama walivyoletwa juzi baada ya mauaji ya Padri,” alisema.

Alisema yeye hakubaliani na msemo wa Serikali wa vita dhidi ya dawa za kulenya, isipokuwa vita anayoinoa yeye ni vita ya rushwa.

“Kama viongozi hawa wameshindwa kuwakamata wahusika wanaosema wanawajua, basi wanahusika kuchukua rushwa au la sivyo, hata mawaziri na wenyewe wanahusika na biashara hiyo.

“Ninyi wabunge kama mnataka pesa zimiminike kwenye halmashauri zetu, tupambane na rushwa na dawa za kulevya,’ alisema.

Lugola alisema, Serikali haiwezi kupambana na rushwa bila kuwekeza fedha na kwamba isiwalaumu polisi kwa vitendo vya rushwa badala yake wawaongezee mishahara.

“Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato (TRA), waliongezewa mishahara ili wasichukue rushwa kwa nini Serikali inapata kigugumizi kuongeza mishahara ya polisi?

“Mimi sitaunga mkono hoja hii kama Serikali haitaanzisha mfuko maalumu katika Jeshi la Polisi ili kuboresha maslahi yao,” alisema.

Mbunge huyo pia alilalamikia kitengo cha maafa kwa kudai kuwa kitengo hicho ni ulaji wa Serikali.

Alisema Serikali inasubiri wananchi wa jimbo lake wakumbwe na njaa ndipo wajenge miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji kutoka Ziwa Victoria hadi Mwibara.

Mazishi ya vigogo yatengewa Sh bil. 1

Mbunge aliishangaa Serikali kutenga Sh bilioni 1 katika bajeti ya ofisi hiyo, kwa ajili ya mazishi ya viongozi wa kitaifa, huku huduma za wananchi zikizorota.

“Na hii Sh bilioni 1 iliyotengwa kwa ajili ya mazishi ya viongozi wa kitaifa, ni wizi mtupu, wabunge wenzangu tusukubaliane na maneno matamu ya bajeti hii,” alisema.

Kwa upande wake, Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Kessy (CCM) alisema wabunge wanapoteza muda kujadili bajeti ambayo sehemu kubwa imejaa ahadi za wafadhili.

“Hapa tunapiga kelele kupitisha bajeti tukienda kwenye halmashauri fedha hakuna, wafadhili hawajaleta, kwani tulidai uhuru kutegemea fedha za wafadhili?” Alihoji.

Aidha, alizitaka halmashauri zisiadhibiwe kwa kutopelekewa fedha, kutokana na ubadhirifu unaofanywa na watumishi wachache.

Alisema kuziadhibu halmashauri ni kuwaonea wananchi wasio na hatia kwa kosa la watendaji wachache waliopelekwa katika halmashauri na Serikali yenyewe.

Kessy pia alitaka Serikali kujenga uwanja wa ndege katika jimbo lake, ili kumaliza tatizo la maji na kujenga barabara zilizopo kandokando ya Ziwa Tanganyika kwa kuwa hali zake ni mbaya.

CHANZO:MTANZANIA
 
Aache kutishia nyau huyo -----, hawa jamaa walishatuona sisi mazuzu siyo? Kwanini atishie badala ya kuwalipua moja kwa moja?
 
Pole yake atamfuata prof saitoti

Mimi nadhani ni sahihi kusema atamfuata marehemu Amina Chifupa.

Nchii hii ukigusa wakubwa ni either ung'olewe meno na kucha au wanaweza "wakakukolimba"

Hata hivyo,hali hii isiwe kikwazo cha kudai haki na mabadiliko.
 
Mimi nadhani ni sahihi kusema atamfuata marehemu Amina Chifupa.

Nchii hii ukigusa wakubwa ni either ung'olewe meno na kucha au wanaweza "wakakukolimba"

Hata hivyo,hali hii isiwe kikwazo cha kudai haki na mabadiliko.

likifika suala la dawa za kulevya huwa linaniumiza kichwa sana.....Amina alijitosa wakamuwahi,mkulu naye akadakia kama kawaida yake akaenda mbali akasema majina ya wahusika anayo tena wengine ni Watumishi wa Mungu atawataja hadharani mda si mrefu........cha ajabu mkulu yuko hai anadunda na orodha ya wauza unga mitaani naye tuseme amenywea,KANGI LUGOLA amejitosa I bet anaigiza hafiki popote kama kweli bomu la china la kutaka kunyonga mtu lilikuwa la kweli ndugu.
 
Lugola ana historia zake. Hakuna mtu wa kumfanya nini wala nini. Na analolisema anamaanisha. Yule mzee ni wa ukwlei. Tatizo yuko ccm.
 
Labda kama anamaanisha vigogo wabwia unga a.k.a mateja hususani wa pale Kinondoni na TMK!
 
Mkuu wa kaya kama sijakosea 2009 au 2010 wakati wa hotuba za mwezi aliwahi kusema ana orodha ya vigogo wa unga na atawataja mpaka leo sijasikia lolote sijui imepotea
 
hawataki tu kuwakamata hao wauza unga, njia rahisi mno ni kuzitumia serikali za mitaa, yani unakamata kuanzia vibaka mpaka majambazi, mateja mpaka madealer na hao ndiyo watakuonyesha wanapata wapi. vyanzo vya kuwajua vingi ,lakini havitumiwi
 
Anajitafutia kifo cha lazima huyu gamba
 
huyu si alikuwa askali tena ocd pale magomeni anayajua majina yote
 
Sasa huyu Mbunge anatafuta lake.tutakula wapi kaka wacha tuuze unga,sukari

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Huu ndio upuuzi mwingine wa wanasiasa wa Tanzania, kama anawajua anangoja nini sasa muda wote huo

silly political mileage mongering
 
Kama anawajua si awataje? Ila awe makini..
RIP Amina Chifupa
RIP George Saitoti
 
DHAIFU naye si alishawahi kutamka kwamba ana list ya wauza unga wote nchini lakini hadi hii leo bado kaikalia!!!
 
Back
Top Bottom