Mbunge Nicholaus Ngassa: "UWT ni nguzo imara ya chama"

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,895
940
đź“Ť Igunga, Tabora - MBUNGE NICHOLAUS NGASSA: "UWT NI NGUZO IMARA YA CHAMA"

Mbunge wa Jimbo la Igunga Mhe. Nicholaus George Ngassa ameipongeza Jumuiya ya Wanawake (UWT) Wilaya ya Igunga kwa kuanza ujenzi wa nyumba ya makazi ya Katibu wa UWT Wilaya.

Mheshimiwa Ngassa ( MB) ametoa pongezi kwa Umoja wa Wanawake (UWT) wakati akikabidhi ramani, michoro na matofali elfu moja kwa Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ajili wa kuanza ujenzi;

"... UWT umoja wenu na mshikamano wenu, unaifanya Jumuiya yenu kuwa nguzo imara kwenye Chama chetu. Mama zangu na Dada zangu endeleeni kushikamana na sisi tutawapa ushirikiano wa kutosha ndio maana Leo nimeanza kutekeleza ahadi zangu kwenu kwa kuwakabidhi Ramani ya jengo na matofali elfu moja ya saruji kwa ajili ya kuanzisha ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Wilaya..."

Hafla ya makabidhiano ya Ramani, michoro na matofali imehudhuriwa na Waheshimiwa Madiwani wa Viti Maalum na Viongozi wa Umoja wa Wanawake (UWT) wa Kata na Matawi.

"Kazi na Maendeleo"

Imetolewa na:
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Igunga

indexqwe.jpg
indexwerty.jpg
indexrtyuio.jpg
indexrtyui.jpg
indexiopk.jpg
 
Back
Top Bottom