Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,428
Habari kubwa ni kwamba Mbunge wa Jimbo la Ngara Mh Ndaisaba George Ruhoro akiwa Bungeni Dodoma amewasemea wananchi Zaid ya 1,200 walioguswa na mradi wa Tembo Nickel
Ruhoro ameishukuru Serikali kwa kulipa zaidi ya Billion 26 kwa wananchi hao ijapokuwa fedha hiyo imekwisha tumika ingali uhamisho wa wananchi hao haujakamilika.
Ruhoro ameomba mambo yafuatayo;
1. Serikali iisimamie Kampuni ya Tembo Nickel ili ikamirishe ujenzi wa nyumba za makaazi ambapo wananchi hao watahamishiwa. Kujenga nyumba tano za mfano niucheleweshwaji wamakusudi kwa kuwa tasnia ya Kihandisi inawezesha kuona jengo litakavyokuwa hata kwa kutumia teknolojia ya 3D.
2. Serikali iikumbushe Tembo Nickel kutoa ruzuku ya Chakula kwa familia zitakazo hamishwa ambazo zimezuiliwa kuendeleza maeneo ambayo yalikwisha fanyiwa tathimini.
3. Serikali iishauri Tembonickel kulipa angalau 20% ya fedha kutoka kwenye 40% ya fedha iliyotunzwa kutoka kwa kila mguswa
Mh RUHORO amesema kuwa kuendelea kuweka waguswa bila kuwapa hizo huduma kutaongeza gharama za mradi wa Tembonickel napengine kuifanya nickel ya Ngara kuwa na gharama kubwa kwa kuwa wananchi watao mba fidia iongezeke.
Wenu
Ernest Ruhugu
Katibu wa Mbunge
Jimbo la Ngara