Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,069
- 34,839
Mmh. Huyu mbunge ana sura mbilimbili, je anawaunga mkono wananchi madai yao? Na je wakati wa kuwasilisha bajeti ya nishati na madini je aliunga mkono hotuba ya kambi rasmi ya upinzani? Kama sivyo wanamtwara wasimtegemee huyu mbunge kwao ni mzigo!
mbona kabla ya vurugu akuyasema hayo?na kwa mujibu wa aliyoyasema mbunge wa ccm Mtwara walichokuwa wanaitaji wana mtwara yeye kama mbunge alishindwa kuieleza serikali?na serikali kuyasema hayo baada ya vurugu inamaana walikuwa hawaelewi wana mtwara wanataka nini? sasa ili kumaliza vurugu kabisa serikali inatakiwa kujenga kwanza hicho kiwanda cha kuchakata gesi kabla ya bomba, lakini sidhani kama watakubaliana na hilo kwa sababu serikali haina nia ya kujenga kiwanda watajifanya hili hawalielewiWaziri Mkuu Pinda awasilisha maombi kwa Maaskofu
Kuzindua ujenzi kiwanda cha sementi leo
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (Kushoto), akiongozana na Mbunge wa Mtwara Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hasnein Murji baada ya sherehe za kusimikwa kwa askofu mpya na wa kwanza wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki Mtwara zilizofanyika mjini Mtwara jana.
Mbunge wa Mtwara Mjini, Hasnain Mohamed Murji, amesema wananchi wa Mtwara hawazuii gesi asilia kusafirishwa kwenda Dar es Salaam, bali wanachotaka ni kuwapo kwa mchanganuo wa jinsi watakavyonufaika na mradi huo.
Mbunge huyo alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotaka kujua msimamo wake juu ya suala hilo, ambalo awali aliwahi kulizungumzia.
Mahojiano hayo yalifanyika baada ya kumalizika kwa ibada ya kumsimika Askofu wa kwanza Dayosisi ya Kusini Mashariki wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Lucas Mbedule na Msaidizi wake, Yeriko Ngwema.
"Kimsingi, hakuna anayekataa gesi asilia ya Mtwara kutoka, kinachogombaniwa ni manufaa, serikali iweke wazi sera, mrabaha na uhakika wa ajira kwa vijana ndipo iendelee kutandaza bomba la kutoa gesi," alisema.
Alisema viashiria vibaya vinaonekana kwa kampuni ambazo zimeanza kazi katika kijiji cha Madimba eneo la Msimbati, ambako patajengwa mtambo wa kuchakata gesi asilia.
Alisema kwenye eneo hilo ajira za udereva na ulinzi ambazo hazihitaji wasomi waliobobea zimepewa watu wa maeneo mengine huku wana Mtwara wakiwa na sifa na tatizo kubwa la ajira.
Murji alibainisha kuwa wananchi wa Mtwara wanajifunza kutoka mkoa wa Lindi, ambako inapatikana gesi ya Songosongo inayosafirishwa kwenda Dar es Salaam kwamba imepita miaka tisa, lakini wananchi wa eneo hilo na mkoa hawanufaiki kwa kiwango kilichotarajiwa.
Alisema tatizo kubwa lililopo kwa sasa ni elimu kwa wananchi ambao wanaamini ujio wa gesi hiyo ndiyo mwisho wa matatizo yao bila kujua kuna changamoto kubwa ambazo wanapaswa kukabiliana nazo.
Hata hivyo, aliishukuru serikali kwa kuonyesha jitihada katika kuwasikiliza wananchi na Bunge kuunda kamati ya wabunge kwenda Mtwara kusikiliza madai ya wananchi na kujionea hali halisi.
Katika ibada hiyo ambayo iliongozwa na Mkuu wa KKKT, Askofu Dk. Alex Malasusa, mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, na ilihudhuriwa na maaskofu wa Dayosisi nyingine za KKKT, viongozi wa serikali na siasa na wengine kutoka ndani na nje.
PINDA: GESI ITAKWENDA DAR
Pinda akitoa salamu za serikali katika ibada hiyo, alisema msimamo wa serikali wa kutoa gesi hiyo kwenda Dar es Salaam ili itumike kwenye viwanda mbalimbali uko pale pale.
Alisema pamoja na usafirishaji wa gesi hiyo kwa bomba serikali itajenga viwanda mbalimbali, mtambo wa kuchakata gesi na kituo cha Liquid Refine Gas (LRG), ambavyo vitatoa ajira kwa wingi kwa wananchi wa Mtwara na wananchi wengine.
Pinda alisema leo anatarajia kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha saruji ambacho baada ya kukamilika kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani milioni tatu kwa mwaka na kuajiri wafanyakazi takribani 1,000 kiwandani na 9,000 wataajiriwa kwenye sekta binafsi kutokana na saruji itakayozalishwa.
Alisema Mei 22, mwaka huu, ilikuwa ni siku ya kuweka jiwe la msingi katika eneo litakalojengwa mtambo wa kuchakata gesi, lakini kutokana na vurugu,wataalamu waliokuwa wakijenga walikimbia na kwamba watarudi kuendelea na kazi.
KAMPUNI 45 KUWEKEZA MTWARA
Aidha, alisema hadi sasa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kina maombi takribani 45 ya kampuni zinazotaka kuwekeza mkoani humo kikiwamo kiwanda cha mbolea na bidhaa za plastiki.
"Kugundulika kwa gesi asilia kuna faida nyingi zitakazopatikana kama kuboreshwa kwa huduma za jamii kutokana na kodi ya huduma, kuwapo kwa umeme na maji safi," alifafanua na kuongeza kuwa kampuni zitakazojihusisha na utafutaji wa gesi asilia zinashiriki kikamilifu katika kujenga miundombinu ikiwamo barabara, viwanda na kufadhili miradi ya elimu, afya na mafunzo
CHANZO: NIPASHE
Mkuu gogo la shamba Huyu Mbunge ni wa chama tawala atafanya kitu gani ili aweze kuwaridhisha Walimchaguwa kushika huo wadhifa wake? Anatumia maneno matamu ili aweze kuifurahisha Serikali yake na Wananchi wake waliompa kura wawe na imani nae lakini hakuan kitu hapo ni uongo mtupu.mbona kabla ya vurugu akuyasema hayo?na kwa mujibu wa aliyoyasema mbunge wa ccm Mtwara walichokuwa wanaitaji wana mtwara yeye kama mbunge alishindwa kuieleza serikali?na serikali kuyasema hayo baada ya vurugu inamaana walikuwa hawaelewi wana mtwara wanataka nini? sasa ili kumaliza vurugu kabisa serikali inatakiwa kujenga kwanza hicho kiwanda cha kuchakata gesi kabla ya bomba, lakini sidhani kama watakubaliana na hilo kwa sababu serikali haina nia ya kujenga kiwanda watajifanya hili hawalielewi
na hao wakubwa wanakaa na kusikiliza kumbe wanaadaa watu,wanasema wachina walikuwa waanze kuchenga kiwanda lakini walikimbia baada ya vurugu, je? watakaporudi wataanza kujenge kiwanda au wataendelea na ujenzi wa Bomba? hapo tutegemee kupata jibu kama la huyo mbunge yaani kubabaishaMkuu gogo la shamba Huyu Mbunge ni wa chama tawala atafanya kitu gani ili aweze kuwaridhisha Walimchaguwa kushika huo wadhifa wake? Anatumia maneno matamu ili aweze kuifurahisha Serikali yake na Wananchi wake waliompa kura wawe na imani nae lakini hakuan kitu hapo ni uongo mtupu.
Mkuu gogo la shamba Ndio maana ikaitwa neno Siasa ni uongo wa hali ya juu Mkuu tutaongopewa mpaka wakati wa uchaguzi ujao wa mwaka 2015 tuwachague hao hao wanao tuongopea, tumegeuka ni vipofu tunaongozwa na vipofu wenzetu mwisho wake tutatumbikia shimoni kama alivyosema Bwana Yesu kristo. Waacheni hao Viongozi Vipofu na kiongozi kipofu akimuongoza kipofu mwenzie watatumbia wote wawili shimoni. Tungojee kutumbukia shimoni mkuu.na hao wakubwa wanakaa na kusikiliza kumbe wanaadaa watu,wanasema wachina walikuwa waanze kuchenga kiwanda lakini walikimbia baada ya vurugu, je? watakaporudi wataanza kujenge kiwanda au wataendelea na ujenzi wa Bomba? hapo tutegemee kupata jibu kama la huyo mbunge yaani kubabaisha