Mbunge Massele aumbuliwa mbele ya Rais Magufuli leo Shinyanga

kasenene

JF-Expert Member
Jun 6, 2008
1,632
2,413
Ile desturi ya Magufuli ya kuwaita viongozi wa kisiasa waje kutoa malalamiko ya majimbo yao pale anapokuwa anahutubia Wananchi, hatimaye leo makubwa yamemtokea puani Mbunge wa Shinyanga mjini pale JPM alipomuita kuja kuelezea kuhusu changamoto kuhusu bei ya huduma ya kupata maji katika mji wa Shinyanga na aeleze ukweli kama bei ipo juu kuliko mikoa yote kama alivyokuwa amemweleza mapema kabla ya mkutano.

Mbunge kwa Mikogo akasema kuwa Shinyanga huduma ya kulipia maji ipo juu kuliko hata Dar es Salaam na wamekuwa wakibebeshwa gharama za watumiaji wa mikoa inayoizunguka Shinyanga. Baada ya kusikia hayo malalamiko JPM akamuita Mhandisi wa Maji wa Mkoa wa Shinyanga kuthibitisha kauli ya mbunge, Mhandisi bila kupindisha pindisha na inaonekana alikuwa kajipanga kweli kweli kwa data akamsomea gharama za ulipiaji maji katika mikoa nane Shinyanga ikiwa mojawapo na ikaonekana kuwa Wananchi wa Shinyanga ndio wanaolipia kiasi kidogo cha maji kuliko mikoa iliyotajwa.

Ikumbukwe kabla ya kuwaita jukwaani hao viongozi wawili Magufuli alikuwa ametoa angalizo awali kwa Wananchi kuwa kama bei wanayotozwa wanashinyanga ipo juu basi leo ataishusha iwe kama mikoa mingine na kama ipo chini vile vile ataipandisha pia...Unajua kilichotokea baada ya mhandisi kumuumbua mbunge Wananchi woote kimya JPM akabadilisha ajenda nakushukuru wanakwaya na kwa mapokezi mazuri...Hapa kazi tu!
 
Mbona hajapandisha bei baada ya kuona wanatozwa bei ndogo?
Hahahahaha.
Angepandisha bei na kumtumbua mhandisi kwa kupingana na mbunge hadharani teh teh
 
Mhandisi wa maji asipotumbuliwa basi nitaanza kuheshimu taaluma yangu,mbunge hakuwa na takwimu ametoka kuuguza,na inaonyesha hana ofisi wala katibu,swali lilihitaji jibu fupi tu.Je ni kweli mji wa shinyanga una bei kubwa ya maji kuliko miji mingine Tanzania?
 
Uongozi ni busara,uzoefu nao ni muhimu.
'Wananchi na watanzania' wanaona kauli na vitendo vya viongozi.
Kuna elimu ya darasani,kujifunza kwa wengine na kuna kujifunza kutokana na makosa!!
Watanzania ni wapole sana,Nyerere alisema vitu 4 muhimu ili tuendelee:
1.uongozi safi
2.Ardhi
3.Watu
4.siasa safi
Kuna hili la kujifunza kwa wengine!,
 
Back
Top Bottom