Mbunge Magdalena Sakaya: Fast Jet ni wezi, wezi kabisa

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,969
Mbunge Magdalena Sakaya amedai kuwa kampuni ya Fast Jet inayotoa huduma za usafiri wa ndege ni wezi kwa kuwa huduma zao ni ghali sana, mfano begi unalipia 200,000, maji ya kunywa ya nusu lita unauziwa kwa 3,000.

Ni wezi sana hawa jamaa, ata matangazo yao, bei wanayotangaza mitandaoni ni tofauti na bei halisi
 
Si apande basi, kwani lazima kupanda ndege? ukute hata jimbo analotokea hakuna hata kiwanja cha ndege cha kutua hiyo fastjet (Kaliua - Tabora) sijui anatetea watu wa jimbo gani, tuna matatizo ya msingi wao wanalalamikia starehe, hiyo fastjet safari za ndani hazizidi saa 1 na nusu angani na hulazimishwi kununua kitu ni hiyari yako. HYO MALALAMIKO ILITAKIWA YAWE YANATOLEWA NA WABUNGE WA CCM HAPO TUNGESEMA YANALINGANA NA AKILI ZAO SASA HAWA WA UKAWA, HII NI AIBU.
 
mbunge magdalena Sakaya amedai kuwa kampuni ya Fast Jet inayotoa huduma za usafiri wa ndege ni wezi kwa kuwa huduma zao ni ghali sana, mfano begi unalipia 200,000, maji ya kunywa ya nusu lita unauziwa kwa 3,000

Hivi siku hizi kuna Tume ya Bei ya kupanga bei za tiketi za ndege? Huyu mbunge vipi? Ndege ziko nyingi tu hadi za kukodi si lazima apande hiyo ndege.
 
Co kweliii nishanufaika na punguzo kubwa la bei wanazotoa from/ Kilimanjaro to Mwanza...Wako njemaa sana hawa jamaaa
 
Acha uwongo.Book online halafu lipia kwa Tigo pesa au Mpesa uone.Bei zao ziko wazi.Tena ziko wazi mno.Mimi mwenyewe sijawahi kanyaga kwa ajenti wala ofisi yoyote ya kukata tiketi.Ninakata online na kulipia kwa tigo pesa au mpesa.

hizo za online ziko juu tofauti ukienda ofice zao
 
Mbunge Magdalena Sakaya amedai kuwa kampuni ya Fast Jet inayotoa huduma za usafiri wa ndege ni wezi kwa kuwa huduma zao ni ghali sana, mfano begi unalipia 200,000, maji ya kunywa ya nusu lita unauziwa kwa 3,000.

Wapi Twiga the Mnyongee??
 
mie mwenyewe kuna siku wamenikera kweli! nililipia elfu 15 ya mzigo wakati nakata tiketi halafu kufika uwanjani wakasema nilipie tena, halafu kibaya zaidi mzigo ulikuwa hata haufiki kilo 10, wehu sana! niliingia kwenye website site nikawachamba japo sijui kama meseji ilikuwa senti au la!
 
Hivi siku hizi kuna Tume ya Bei ya kupanga bei za tiketi za ndege? Huyu mbunge vipi? Ndege ziko nyingi tu hadi za kukodi si lazima apande hiyo ndege.

Wewe kweli nungayembe, hiyo hoja huwezi kuielewa kwani huna shughuli za kukufanya usafiri na ukisafiri unaishia na daladala tuu. Eti tume ya kupanga bei! Kwani hujui kuwa nauli za ndege za ndani ziko monitored na serikali na ni lazima zisiwe za kumuumiza mwananchanayelazimika kutumia usafiri huo?
Kama tume ya bei haipo iweje serikali iwe inaweka bei elekezi? Kwa nini inalalamika sukari ikiuzwa 5000 badala ya 1800 ? Wewe chochote kinachoizungumzia serikali lazima ubishe tuu unaakili kweli wewe au ni mzigo usiobebeka? Kama serikali imeshindwa kulifufua shirika lake la ndege basi yapaswa kusimamia kikamilifu iliowapa leseni kufanya shughuli hizo sio wajifanyie watakavyo kwa vile kuna shida ya usafiri. Hii ni kama wafanyavyo wakati wa X mas kwa mabasi yaendayo mikoani.
 
hizo za online ziko juu tofauti ukienda ofice zao

Si kweli inategemea umekata lini mfano mtu aliyekata tiketi leo online atakuta bei iko juu kuliko aliyekata wiki mbili zilizopita iwe ofisini au mtandaoni.

Mtu aliyekata tiketi hata leo hii ofisini kwa safari kesho bei yake ni tofauti na aliyekata tiketi hiyo wiki tatu zilizopita.Ya aliyekata leo itakuwa juu.
 
mie mwenyewe kuna siku wamenikera kweli! nililipia elfu 15 ya mzigo wakati nakata tiketi halafu kufika uwanjani wakasema nilipie tena, halafu kibaya zaidi mzigo ulikuwa hata haufiki kilo 10, wehu sana! niliingia kwenye website site nikawachamba japo sijui kama meseji ilikuwa senti au la!
Ndugu yangu Chikira Mtabari pole sana na hilo, ila napenda kukushauri unapolipia mzigo wasikilize vizuri sana, pengine walikutajia kilo, kwamba kama mzigo wako hauzidi kilo 5 basi lipia shs 15 elfu zaidi ya hapo utalipa zaidi. Sababu hawa wezi kuweka fixed prise kwenye mzigo. Usafiri wa ndege kwenye mizigo unaendani na uzito, hiyo elfu 15 je nikiingia na bagi la kilo 25 itabaki hiyo hiyo? Kwa hiyo mara nyingi uwe makini, pengine sio kosa lako ila wale walio kupa hiyo bei hawa kutoa maelezo ya kutosha. Au kabla ya kukata tiketi ingia kwenye website yao soma vya kutosha utapata maelezo yote. Sababu kama unakata tiketi online kila kitu unasoma mwenyewe.
 
huduma zao ni ghali sana, mfano begi unalipia 200,000, maji ya kunywa ya nusu lita unauziwa kwa 3,000.

Wabunge hawa nafikiri upeo wao mdogo kuhusu ndege aina ya hizo za fast jet.Ndege hizo zinajulikana kama BUDGET AIRLINE au kiswahili ndege za watu wa hali ya chini.Hizi hutakiwi kuwa na mizigo mizito au mikubwa.Hizi hubeba abiria wengi zaidi na mizigo michache yenye uzito mdogo na ukubwa mdogo.Ukibeba mzigo mkubwa wanakukomesha kwa kukulipisha pesa nyingi kwa kila kilo itakayozidi viwango vyao.Hizi sio sawa na zile ndege za ATC ambazo hubeba hadi matenga ya sangara na SATO toka Mwanza.

Masanduku ya waheshimiwa wabunge tunayajua ni robo kontaina ukipenda kuita.Kubwa halafu zito hilo acha tu.Ukipewa ulibebe kama ni kibarua inabidi umwambie aongeze hela.Hayo masanduku Fast JET kuwakubalia ni kuwahurumia tu wangetaka wangewaambia huu mzigo hatubebi.

Kuwapunguzia abiria gharama bei za vyakula na maji huwa hazimo kwenye tiketi ukitaka chochote utanunua ndani ya ndege.Huduma bure mle ndani ni choo tu.Mtu anayenunua maji ndani ya ndege ni tajiri MKUBWA hizo elfu tatu kwake si kitu.Hulazimishwi kununua waweza kauka hadi unakoshuka maji ukanywe kwenu.
 
Kama tume ya bei haipo iweje serikali iwe inaweka bei elekezi? Kwa nini inalalamika sukari ikiuzwa 5000 badala ya 1800 ?

Kwenye sukari serikali huwa inatoa ruzuku na kusamehe kodi kwa kila kilo ya sukari ina haki ya kutoa bei elekezi.
 
Jamani jamani jamani.... wabunge wetu jitahidini kufanya utafiti wa kina kabla ya kuongea huko bungeni. Magdalena Sakaya ni msomi mzuri kabisa, ameshindwaje kujua 'business model ya low carrierr airline kama Fastjet? Magdalena anasema begi unalipia 200,000 lakini hasemi begi lina uzito gani? Na pia alifanya booking siku aliyosafiri au kabla?
 
Si kweli inategemea umekata lini mfano mtu aliyekata tiketi leo online atakuta bei iko juu kuliko aliyekata wiki mbili zilizopita iwe ofisini au mtandaoni.

Mtu aliyekata tiketi hata leo hii ofisini kwa safari kesho bei yake ni tofauti na aliyekata tiketi hiyo wiki tatu zilizopita.Ya aliyekata leo itakuwa juu.

inshu sio unakata tiketi ya lin inshu ni kwamba bei ya online ni juu sana tofauti na ukienda office zao sasa wewe utajuaje wakati huwa hukanyagi office zao! wakati unacheki mtandao bei ya tarehe fulani ni tsh. 147,000 ukienda office zai unakuta bei ya trh hiyohiyo muda muda huohuo ni tsh. 88,000. acha ubishi chukua hii uanze kuokoa pesa ulizokuwa unapoteza
 
Wapi Twiga the Mnyongee??

Twiga hivi karibuni analetewa mabawa matatu. Ili angalau aweze kupeperuka kidogo.
Swali la kujiuliza ni kwamba mara nyingi twiga huyu mnyonge asiye na makuu amekosa waangalizi wa kumpatia malisho akakua na kuzaliaana.
Mchungaji wa twiga huyu mnyonge amekuwa akikamua maziwa bila kiangalia kama twiga amelishwa majani ya kitosha aweze kutoa mazIwa vizuri.

Je tunaweza kujisahihisha makosa yetu kumnyooshea kidole twiga huyu mnyonge pindi maziwa ya kuadimika na kusahau wema wake pindi maziwa yalipokuwa ya toka kwa wingi.
 
Hivi siku hizi kuna Tume ya Bei ya kupanga bei za tiketi za ndege? Huyu mbunge vipi? Ndege ziko nyingi tu hadi za kukodi si lazima apande hiyo ndege.
Mkuu acha zako mbunge yeye anauwezo wa kupanda ndege yoyote ile ila kasemea wananchi ambao hawana uwezo
 
inshu sio unakata tiketi ya lin inshu ni kwamba bei ya online ni juu sana tofauti na ukienda office zao sasa wewe utajuaje wakati huwa hukanyagi office zao! wakati unacheki mtandao bei ya tarehe fulani ni tsh. 147,000 ukienda office zai unakuta bei ya trh hiyohiyo muda muda huohuo ni tsh. 88,000. acha ubishi chukua hii uanze kuokoa pesa ulizokuwa unapoteza

Ukikata online nakubali kuna gharama za huduma zingine huongezeka ambazo huduma hizo huwezi zipata ofisini.Mfano online unachagua hadi kiti ukae kiti kipi.Ofisini hupewi hiyo huduma.Kuchagua kiti unachajiwa sio bure.Pia waweza check in wewe na mzigo wako online huduma hiyo pia wanakuchaji sio bure.Ofisini unakatiwa isiyokuwa na hayo mengine ndipo urahisi unapokuja mara ingine ila si mara zote.Mimi sipendi usumbufu ndio maana napenda kukata online.
 
Back
Top Bottom