Mbunge Lusengekile Ampongeza PM Majaliwa kwa Mabadiliko ya Kitaifa

Mbunge Lusengekile Ampongeza PM Majaliwa kwa Mabadiliko ya Kitaifa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,428

MBUNGE LUSENGEKILE AMPONGEZA PM MAJALIWA KWA MABADILIKO YA KITAIFA

Mbunge wa Busega Mkoani Simiyu, Simon Songe Lusengekile, ametoa wito kwa wananchi wa Ruangwa, Mkoani Lindi, kuendelea kumuamini Mbunge wao ambaye pia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, akisisitiza kuwa uongozi wa Majaliwa umekuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo katika Halmashauri mbalimbali nchini.

Akichangia Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu mapema, Alhamisi Aprili 10, 2025, Bungeni jijini Dodoma, Lusengekile amesema kila mara Waziri Mkuu anapofika kwenye Halmashauri yoyote, huacha alama kwa kuleta mabadiliko ya kiutendaji, hali ambayo imekuwa na matokeo chanya kwa utoaji wa huduma kwa wananchi.

Katika mchango wake, Lusengekile pia amewasilisha maombi maalum kwa Waziri Mkuu, akiiomba serikali kuangazia changamoto zinazolikabili Jimbo la Busega. Amesisitiza umuhimu wa kulipatia jimbo hilo watumishi wa afya wa kutosha ili kuendana na kasi ya ujenzi wa vituo vya afya vinavyoendelea Jimboni kwake.

Aidha, amekitaja chuo cha VETA cha Wilaya ambacho kinakabiliwa na ukamilishaji, akiiomba serikali kuhakikisha kinakamilika ili kiweze kutoa mafunzo kwa vijana wa eneo hilo. Mbunge huyo pia amewasilisha ombi la kuondolewa kwa magugu maji katika Mto Lamadi, akieleza kuwa hali hiyo inasababisha mafuriko makubwa ambayo yamekuwa yakiathiri wakazi wanaoishi kandokando ya mto huo.
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2025-04-11 at 12.53.00.mp4
    4.8 MB
Back
Top Bottom