PreGE2025 Mbunge Kihenzile akagua Ujenzi wa Kituo cha Afya Mninga, asisitiza ushirikiano wa Serikali na Wananchi

PreGE2025 Mbunge Kihenzile akagua Ujenzi wa Kituo cha Afya Mninga, asisitiza ushirikiano wa Serikali na Wananchi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

upupu255

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
341
Reaction score
476
Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini na Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile amefanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Mninga.

1742710117300.png
Akizungumza na wananchi waliojitokeza kituoni hapo, Kihenzile amesema kuwa ujenzi wa kituo hicho hadi kukamilika siyo nguvu zake pekee kama mbunge bali ni juhudi kubwa zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan pamoja ni ushirikiano baina ya diwani pamoja na wananchi wa kata hiyo.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mradi huu wa Kituo cha Afya Cha Mninga unatarajiwa kuwahudumia wananchi wapatao 15,795 ambao walilazimika kutembea zaidi ya kilometa 10 kufuata huduma za upasuaji wa dharura kwenye Kituo cha Afya cha Kasanga, Lugoda na Hospitali ya Wilaya ya Mufindi.

1742710133660.png


1742710152106.png


1742710168803.png
 
Back
Top Bottom